Thursday, December 31, 2009

Ni kutokujua kusoma au ukaidi...?


Mfanyabiashara ndogondogo akiuza ndizi katika eneo linalokatazwa kandokando ya barabara ya kuelekea hospitali kuu ya Mkoa wa Dodoma. Lakini kwa nyuma askari nao wakipita na hamsini zao, ingawa bango linalokataza biashara limeandikwa kuwa na amri halali..... Hapo sasa....

Monday, December 14, 2009

Usafiri Wilayani....

Usafiri maeneo ya wilaani si mchezo .... kama unavyoshughudia hapo katika picha nilizonasa kwenye barabara ya Dodoma-Kondoa..... hiyo land-rover 110 imejaza mizigo kupita kiasi huku jamaa wakiwa wanakula upepo juu..... hapa chini ni basi aina ya isuzu journey ..... tingo katoka juu kurekebisha mizigo wakati gari ipo katika mwendo... akabidi aingilie kwa dirishani...

Sunday, December 13, 2009

Ndani ya Dom: Str8Muzik Festival:InterCollege Special 2009

Waliofanya ridhim ziende vyema vilikuwa hivi vichwa...Ma-DJz hawa wakiwa kwa kazi.......
Hip Hop artist toka Kenya..... Nonini... al-mahruf kama..Genge.... akichana Keroooro.....

Wazee wa Keroro nao kwa floor wanazidi pagawa.......


Msaanii huyo nae .....Amani Swazagone... alikonga nyoyo za madent.... hapo royal village mjini Dom......

Izo Bizzness na Quick Racker wakifanya mambo kwa stage...... ebana si matani kilele cha Str8Muzik Festival:InterCollege Special 2009 ....'kilinoga kunoga.......'

Str8Muzik Festival;Intercollege Special 2009

Joe Makini a.k.a Mwamba wa Kaskaz.. akimwaga mistari wakati wa music bash.... Str8Muzik Festival:InterCollege Special katika hotel ya Royal Village mjini Dodoma usiku wa Jumamosi (Dec 12) kuamkia J'2 (Dec 13).
Mzee wa Shikide... Dully Sykes a.k.a Mr. Misifa akibembea na 'bamutu bataokota benyewe kunyavu.....'

Crowd ilikuwa hot... ukizingatia madent wa colleges za Dom... plus kilauri.... ilikuwa balaa......

Albert Mangwair....mwana wa East Zoo.... akiwaambia 'nipeni..nipeni deal masela.... nikamate mahela...'

Ndo hapo alipowachanganya wana East Zoo........

Sunday, October 18, 2009

Moh Trans yapata ajali

Abiria wakishuka kutoka katika basi la Mohammed Trans lenye namba za usajili T779 AWH katika kituo cha Mabasi Mjini Dodoma Jumatano (14/10/2009) usiku. Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma lilipata ajali baada ya kugonga lori katikati ya eneo la Gairo na Pandambili ambapo mtu mmoja alikufa papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Tuesday, October 13, 2009

Mwanamke Anayetoa Machozi ya Damu Kila Anapolia

Rashida Khatoon Sunday, April 19, 2009 4:12 AM
Mwanamke mmoja nchini India amejipatia umaarufu na kuwa gumzo nchi nzima kutokana na hali yake ya kutoa machozi ya damu kila anapolia. Rashida Khatoon mkazi wa mji mmoja kaskazini mwa India, amewashangaza hata madaktari kwa hali yake hiyo ya kutiririka machozi ya damu kila anapolia.

Kwa siku mwanamke huyo humwaga chozi la damu mara kadhaa.

"Sisikii maumivu yoyote, badala ya machozi ya kawaida, damu zinapotitirika ni kitu cha kushangaza" alisema mwanamke huyo ambaye amekuwa gumzo sana nchini India.

Viongozi wa dini wa India wanadai kwamba mwanamke huyo ni miujiza toka mungu.

Kutokana na umaarufu mkubwa aliojizolea mamia ya watu wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa mwanamke huyo kujishuhudia wenyewe kwa macho yao.

Wageni hao wamekuwa wakimmiminia mwanamke huyo na familia yake zawadi kadhaa kila wanapomtembelea nyumbani kwake.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetai...1790150&&Cat=7

Friday, August 28, 2009

Uzembe mwingine bwana... wee wacha tu...!!!

Gari ikiwa imetupwa kiasi cha mita 50 toka mahala ilipogongwa na kiberenge eneo la majengo mjini Dodoma hivi karibuni wakati dereva akitaka kuwahi kuvuka kabla ya kiberenge hicho kupita.
Baadhi ya mashuhuda wakiangalia gari hilo ambapo hata hivyo hakuna abiria aliyejeruhiwa saaana.....
Mmoja wa walioshughudia ajali hiyo akijaribu kuelezea ilivyotokea....si unajua jinsi tulivyo hodari katika kusimulia.... kama movie vile.....!!!

Thursday, August 27, 2009

Mavituz ya Traffic police huyu.. balaa...!!

Download uone mavitu ya huyu traffic akiongoza magari.....kama angelikuwa bongo.. sidhani kama angelikuwepo hai.....!!!!

Mjihadhari na watu msiowajua mkiwa safarini...!!!

Kijana Meshark Simon akiwa amelala hajitambui jana baada ya kupewa kitu kinachodhaniwa kuchanganywa na dawa za kulevya alipokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma katika basi la Kilimajnaro Line na kuibiwa vitu alivyokuwanavyo ikiwa ni pamoja na simu ya kiganjani na fedha.
Utingo wa Basi la Kilimanjaro Line akijaribu kumuuliza ilivyotokea kijana Meshark Simon. Jamani abiria mjihadhari na watu msiowajuwa mkiwa safarini....!!!

Wednesday, August 26, 2009

Je hii ni mikogo au taabu ya usafiri...?

Watoto wakiendesha baiskeli katika Bara bara ya Bahi mjini Dodoma jana wakiwa wamepakizana katika hali ambayo inahatarisha usalama wao barabarani.

Tuesday, August 25, 2009

Cycle For Understanding mission....

Eric Silverman akipiga picha ya video waliposimama kwa muda katika hoteli ya Dodoma Hotel....
Aaron Bodansky (kulia) na Eric Silverman wakizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma wakiposimama kwa muda wakiwa njiani kuelekea jijini Nairobi Kenya wakitokea Cape Town, Afrika Kusini kwa kutumia baiskeli, katika kampeni yao ya kubadilisha fikra na mtazamo wa wamarekani juu ya Bara la Afrika. Jamaa hawa wawili ambao nao pia ni Wamarekani wamemaliza safari yao hiyo salama bin salmin.
Hapa Aaron Bodansky akielezea jinsi hali ya safari yao ilivyokuwa tangu walipoingia katika mpaka wa Tanzania hadi kufika Dodoma.

Vibuyu

Mwaha akitafuta wateja wa vibuyu katika mitaa ya mji wa Dom..... babu huyu ni kwa miaka mingi sasa hufanya biashara hiyo.....

Sakata la majambazi Dodoma

Majeruhi aliyetwangwa na kitu kizito kichwani na majambazi wapatao sita ambao baada ya kuteka magari matatu likiwemo basi la abiria, walitoroka kwa kutumia gari ya majeruhi huyo. Kwa mujibu wa Polisi, majambazi hayo yaliuawa na wananchi wenye hasira.
RPC wa Dodoma akikagua baadhi ya vitu zikiwemo simu 25 za kiganjani, mkwanja cash Sh1.95, binduki mbili, mapanga na visu walivyokuwa wanatumia majambazi hayo.

Hapa kamanda akizungumza na wakazi wa Dodoma nje ya chumba cha maiti katika hospitali ya mkoa ambapo miili ya watu hao sita ilikuwa imehifadhiwa.

Monday, August 24, 2009

Uzazi wa Mpango

Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Julius Kivelia akiwasilisha mada wakati wa mdahalo wa wazi juu ya masuala ya uzazi wa mpango ulioandaliwa na Engender Health na kufadhiliwa na shirika la USAID mjini Dodoma. Huyu Mtaalam anasema kuwa kasi ya ongezeko la Idadi ya Watu nchini Tanzania ni kubwa mno ijapokuwa ukimwi unaendelea kupunguza watu wengi... na kwamba itaongezeka na kufikia watu millioni 90 katika miaka ya 2035 ikiwa hatua madhubuti za uzazi wa mpango hazitachukuliwa.

Ndo zetu....!!

Mwandesha baiskeli akionesha mikogo yake katika mitaa ya dom......

Nyama choma

Mambo ya Dom ndo haya....Hii ilikuwa wakati wa nane nane.... si wajua wana wa idodomya kwa nyama ndo wenyewe...!!

Ngongoti

Ngongoti akionyesha mikogo yake wakati wa maonesho ya nanenane mjini Dodoma.

Kobe mzee

Baadhi ya wakazi wa Dodoma wakiangalia Kobe mwenye umri wa miaka 151 wakati wa maonesho ya nanenane yaliyomalizika hivi karibuni. Wataalam wanasema kuwa Kobe anauwezo wa kuishi kwa takriban miaka 500.

Hongera

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. James Nsekela akimkabidhi mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Kongwa Debora Hongole Baiskeli ikiwa ni zawadi ya usindi katika mitihani ya majaribio kwa masomo ya Hisabati na Sayansi. Zawadi hizo zimetolewa na Benki ya CRDB.

Wednesday, July 1, 2009

Polisi wakamata SMG


Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoani Dodoma (RCO) akionyesha bunduki aina ya SMG yenye nambari NM 181739 iliyokamatwa toka kwa majambazi mjini Dodoma ikiwa na risasi 21. Watu kadhaa wanashikiliwa kuhusiana na matukio hayo ya uhalifu wa kutumia silaha mkoani humo.

Chizi atinga eneo la bunge

Kijana Steven Onesmo (25) aliyetinga kinyume cha taratibu katika eneo la viwanja vya bunge mjini Dodoma na kutishia kushambulia walinzi kwa kisu akidhibitiwa na wanausalama.
Hapa akitiwa katika londo la wana usalama kuelekea kituoni...

Shughuli ya kumpakia haikuwa ndogo.... kijana hiyo ambaye inasadikiwa kuwa ni chizi alileta maroroso mno.,...

Azaki bungeni maonesho

Meneja Habari wa umoja wa mashirika yasiyo ya kiserikali (TANGO) Zaa Twalangeti (kulia) akitoa maalezo wa baadhi ya watu waliotembelea banda ya asasi hiyo wakati wa maonesho ya asasi za kiraia katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.

Mbilia alivyoiwapagawisha waheshimiwa

MbiliaBel akionesha mauno alipotumbuiza waheshimiwa katika viwanja vya jengoni mwao mjini idodomya.
Hapa akiweka madoido katika wimbno wake mpya 'mobali ya bebe'

Hapa akicheza na waheshimiwa wakati wa onesho hilo......

Spika naye yumoo.....!! hapa ni baada ya kuombwa na mbilia kupanda kwa stage....

Maisha plus watinga bungeni

Mshindi wa shindano la onesho la luninga la Maisha Plus Abdul (kulia) akiwa na watayarishaji wa shindano hilo wakifurahia jambo na Naibu waziri wa Fedha Omar Yusuf Mzee (kushoto) wakati walipotembelea bungeni mjini Dodoma jana. Katikati ni Mbunge wa Mchinga Mudhihir Mudhihir.

Friday, June 5, 2009

Vidosho wa Miss Dom


Warembo 10 watakaopanda jukwaani leo kuwania taji la Miss Vodacom Dodoma wakiwa katika mazoezi.


Friday, May 22, 2009

Mwakyembe kanusurika Mzinga wa namna hii...!!!

Gari aina ya Land Cruiser ambalo Mbunge wa Kyela Dr. Harrison Mwakyembe alimokuwa akisafiria kutoka Kyela kwenda jijini Dar es Salaam likiwa katika eneo lililopata ajali mkoani Iringa jana.... Kwa kweli mzinga adi cruiser katika hali hii inaonyesha kuwa ilikuwa moto chini kinoma...... Hivi ajali hizi za mara kwa mara kwa waheshimiwa hawa ni kutokana na mwendo kasi... ubovu wa magari... kutokuwa makini kwa madereva.... ama.....mkono...wa m2..!!?

Thursday, May 21, 2009

Majambazi Dom wala Sh80

Polisi wakiwasili eneo la tukio muda mchache baada ya watu wanne kupora kiasi cha Sh80 toka kwa mfanyabiashara mwenye asili ya kiasia katika moja ya vituo vyake vya kuuza mafuta mjini Dodoma mwanzoni mwa wiki...
Hapa wakipata maelezo ya awali kutoka kwa watu walioshuhudia tukio hilo jinsi mchezo ulivyochezwa mchana majira ya saa sita hivi...
Hapa wakiangalia maganda ya risasi zilizofyatuliwa na majambazi hao ili kutisha wananchi wasilete longolongo....
Gari lililotumiwa na watu hao wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi likiwa limetelekezwa eneo la makole mjini Dodoma....
Hapa mdosi aliyeporwa cash akipelekwa wodini kutoka chumba cha upasuaji katika hospitali ya mkoa alipopekekwa kwa matibabu baada ya kutwangwa shaba ya kisigini mguu wa kushoto.... mdodi mwenzie akiwaka kutotaka tukio hilo lisirekodiwe na kuwekwa katika kumbukumbu zatu....