Friday, April 3, 2009

Daladala yawaka moto.....

Baadhi ya wakazi wa eneo la Majengo mjini Dodoma wakiangalia gari aina ya Totota Hiace lenye namba za usajili T201ABC lililoteketea kwa moto juzi. Walioshughudia ajali hiyo ambayo hivyo hakuna mtu aliyejeruhiwa wameeleza kuwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme........


Hapa viti kushneikgh....tukauze vyuma chakavu......

Kifo hiki kinamashaka...!!!

Baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamelizunguka gari ya polisi iliyobeba mwili wa mfanyabiashara maarufu mwenye asili ya kiasia, Karim Thawer maarufu kwa jina la Saldina huku bado hawaamini kama kweli katutoka......
Wananchi wakisaidiana na askari kuweka mwili wake kwenye gari(juu)..... (chini) mwili ukitolewa ndani ya duka ambako ndiko kuna ofisi yake......

Hivi ndivyo alivyokutwa marehemu Karim Thawer akiwa ofisini kwake huku amekwisha aga dunia..... Kulikuwa na vitu vyeupe mithili ya povu na mezani pake palikuwa na funguo zake mbalimbali......hotpot ilitokuwa na msosi kiaina... pembeni yake kuna makasha ya dawa... Haikuweza kufahamika mara moja nini kilikuwa chanzo cha kifo chake.... Mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi....