Sunday, October 18, 2009

Moh Trans yapata ajali

Abiria wakishuka kutoka katika basi la Mohammed Trans lenye namba za usajili T779 AWH katika kituo cha Mabasi Mjini Dodoma Jumatano (14/10/2009) usiku. Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma lilipata ajali baada ya kugonga lori katikati ya eneo la Gairo na Pandambili ambapo mtu mmoja alikufa papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Tuesday, October 13, 2009

Mwanamke Anayetoa Machozi ya Damu Kila Anapolia

Rashida Khatoon Sunday, April 19, 2009 4:12 AM
Mwanamke mmoja nchini India amejipatia umaarufu na kuwa gumzo nchi nzima kutokana na hali yake ya kutoa machozi ya damu kila anapolia. Rashida Khatoon mkazi wa mji mmoja kaskazini mwa India, amewashangaza hata madaktari kwa hali yake hiyo ya kutiririka machozi ya damu kila anapolia.

Kwa siku mwanamke huyo humwaga chozi la damu mara kadhaa.

"Sisikii maumivu yoyote, badala ya machozi ya kawaida, damu zinapotitirika ni kitu cha kushangaza" alisema mwanamke huyo ambaye amekuwa gumzo sana nchini India.

Viongozi wa dini wa India wanadai kwamba mwanamke huyo ni miujiza toka mungu.

Kutokana na umaarufu mkubwa aliojizolea mamia ya watu wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa mwanamke huyo kujishuhudia wenyewe kwa macho yao.

Wageni hao wamekuwa wakimmiminia mwanamke huyo na familia yake zawadi kadhaa kila wanapomtembelea nyumbani kwake.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetai...1790150&&Cat=7