Sunday, March 28, 2010

Usiendeshe karibu na lori lilobeba kontena.... Isijekuwa Kama Kibamba

Lori lilobeba kontena likiwa limepiga chini katika makutano ya barabara......huko mamtoni(ila sio kwa aziz ali wala mtongani).....
Madereva mnatahadharishwa kutoendesha karibu na malori ya namna hii... hususan hapa kwetu bondo salidalama..... mengi ya makontena hayo huwa hayajafungwa ipasavyo..... hiii inanikumbusha ileee ajali ya kimara miaka iileeee.... kipanya (sio masoud) kilivyominjwa na kontena...... hebu endelea kuangalia hizo pix za chini......zimeorijineti toka fun&info@letalites.nets.............

Ajali nyingine majuu kama ya kibamba

Moja kati ya magari mawili yaliyoangukiwa na kontena lililokuwa limebebwa na lori......
Waokoaji wakitafuta mbinu ya kuwachomoa walionasa na wakati huo huo kuwapa huduma ya kwanza........
Hapa ni ka-kiganja tu kanaonekana......
Waokoaji wakimpa huduma ya kwanza moja ya wahanga wa ajali hiyo......
Picha hizi nimetumiwa ktk mail na mdau john mwaipopo... ila zinanesha onesha kama zimeorijineti toka fun&info@letalites.nets.............

Ajali ya Kibamba

Ingawa ajali haina kinga.... lakini hii ni nomaa mazee.....
Sijui tumlaumu Dereva....... au barabara...... au gari lenyewe......????

Wednesday, March 24, 2010

Chopper ya Chadema katika anga za Dom

Helikopta inayotumiwa na chadema katika operesheni sangara ikiwa katika anga za Dodoma... imekuwa ni kivutio kikubwa kwa wakazi wengi wa vitongoji.....

Chadema na Operesheni Sangara Dodoma

Helikopta ikiwasili maeneo ya Kibaigwa wilayani Kongwa...
Wakazi wa Kibaigwa wakiizunguka ....... wengine wanaishangaa... hawajawahi kuiona kwa karibu....

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akipokelewa kwa shangwe....


Mpiganaji Mbowe akimwaga sumu jukwaani......

Sumu zikiwaingia vyema wananchi hawa.......

Maadhimisho Siku ya Hali ya Hewa Duniani

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Beda Lagule akirusha pulizo ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Ndege mjini Dodoma tarehe 23 March 2010.
Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Mkoani Dodoma Gaetan Mwikeve akimwonyesha Bw. Beda Lagule baadhi ya vifaa vinavyotumika kupima hali ya hewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Ndege mjini Dodoma




Majukumu kusaidiana babu....

Wakazi wa Dodoma ambao haikufahamika mara moja uhusiano baina yao wakiwa wamebeba watoto wadogo katika hali inayoonyesha kusaidiana majukumu
Majukumu kusaidiana babu....

Tuesday, March 16, 2010

Dear Mama Musica Saundo kunguruma Dom

Wanamuziki wa Bendi mpya ya Muziki wa Dansi .... wenyewe mwaita masebene..... wakishangilia wakati wa utambulisho kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanyika siku ya mkesha wa pasaka......
Waimbaji wakinengua sebene........

Hapo chacha...... Wakisakata mtindo wa 'Makaputura'

Mkurungezi Mkuu wa bendi hiyo.... Josephat Mwashinga akionyesha umahiri wa kucheza sebene wakati wa utambulisho bendi hiyo yenye maskani yake mjini Dodoma......
Hapa "mzee wa makaputura" akionyesha ufundi wa kuimba ingawaje yeye si mwimbaji wa bendi hiyo....... akisaidiwa vocal kwa mbali na rais wa bendi hiyo...Petit Makambo.... mwimbaji na mwanamuziki mkongwe wa siku mingi... toko DRC.....

Siku ya wanawake....

Wakinamama wakimsaidia msichana ambaye alizidiwa wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa mjini Dodoma hivi karibuni.... Mwanamana akiwa na watoto wake wa kike wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa mjini Dodoma.......

Mwanamke na Maendeleo

Mwanadada akizunguka katika mitaa ya mji wa Dodoma akitafuta wateja wa karanga huku akiwa na mwanae mgongoni......Ni Kweli "mwanamke na maendeleo tufanye kazi tusonge mbelee......"??

Mbinu mpya ua ukulima wa Zabibu

Mtaalam wa Kilimo cha Zabibu kutoka Afrika Kusini Dirk Bosman akionyesha mbinu mpya za ukulimwa wa zabibu wakati wa ziara ya mafunzo kwa wakulima wa zabibu katika kijiji cha Mpunguzi mjini Dodoma hivi karibuni. Kwa mbinu hizi mpya, mkuliwa anaweza kuvuna tani kati ya nane hadi 13 kwa ekari ikilinganishwa na tani za sasa tatu hadi tano kwa ekari...... Meneja Mkuu wa Kampuni ya Vinjwaji vikali vya Tanzania Distillers Limited (TDL) akiangalia zabibu zinazolimwa mkoani Dodoma. TDL inampango wa kufufua ao la zabibu mkoani Dodoma ambao hutoa takriban hectolitres 120,000 za malighafi inayotengenezewa Wine aina ya Overmeer pamoja na kinywaji kikali aina ya Value.....

Maadhimisho Wiki ya Nssf yaanza

Wanachama wa shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) wakipata huduma katika ofisi ya mkoa wa Dodoma ikiwa sehemu ya ni maadhimisho ya wiki ya shirika hilo nchini kote.
Ngoja nikuandikishe ndugu...... uchukue kadi yako.....nawe uwe mwanachama....

Glaukoma yaleta upofu kimya kimya.....

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, John Tupa akimvisha miwani Kaundime Seleman wakati wa maadhimisho ya kimkoa ya siku ya Glaukoma Duniani mjini Dodoma hivi karibuni. Mkoani Dodoma pekee takriban watu kati ya 10,000 na 12,000 wamebainika kuugua ugonjwa huo ambapo kati ya hao wagonjwa kati ya 1,500 na 2,000 wamepata upofu kutokana na glaukoma.
Hapa Mkuu huyo wa Wilaya akipimwa uwezo wa jicho kuona taswira na mtaalam wa tiba za macho wakati wa maadhimisho hayo.....