Wednesday, May 26, 2010

Sheria Mkononi......

(PICHANI CHINI) Askari wa kikosi maalum cha polisi cha (Anti-Robbery) kwa kiswanglish…(Shangazi Jambazi) mkoani Morogoro akimsikitikia kijana (aliyelala chini) baada ya wananchi wenye hasira kumpa kichapo kikali kwa tuhuma za kuiba baiskeli katika mtaa wa Azimio kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro…....(PICHANI JUU) ..Hata hivyo kijana hiyo hatoweza kushughudia fainali za kombe la dunia mwezi ujao… kwani ndo keshaaga dunia…Hapo akipakizwa katika Londo la Polisi kuelekea mochwale….
Picha hizo kwa hisani ya mdau Juma Mtanda… unaweza kumcheki katika http:/jumamtanda.blogspot.com

Vikundi vya uhamasishaji vyaanza ibuka ..uchaguzi huo waja...

Duuu.. kumbe hawa jamaa wanafani nyingi.......Katibu wa fedha na Uchumi wa CCM Taifa, Amos Makala akitwanga drums ambazo ni moja kati ya vyombo vya muziki vyenye thamni ya Sh10.2 milioni alivyowakabidhi kwa kikundi cha burudani na uhamasishaji cha ‘Sultani Dot Com’ kilichopo kata ya Sultani, manispaa ya Morogoro, Picha kwa hisani ya Samuel Msuya.

Mo Ibrahim kumtangaza rais bora Afrika 2010


Taasisi ya Mo Ibrahimu inatarajia kumtangaza kiongozi bora mstaafu barani Afrika kwa mwaka 2010 ambaye alichaguliwa kidemokrasia na akaiongoza nchi yake kwa kwa mafanikio katika misingi ya utawala bora.

Kiongozi huyo atajulikana Juni 14 na atakuwa wa tatu kufanikiwa kupata tuzo hiyo inayoandamana na donge nono la papo hapo la dola 5 milioni za Kimarekani (sawa na takriban Sh7.3 bilioni za Kitanzania).

Tanzania ina marais wastaafu wawili, Benjamini Mkapa aliyeongoza serikali ya awamu ya tatu (1995-2005) na Ali Hassan Mwinyi, awamu ya pili (1985-1995).

Kwa mujibu wa taarifa Ilioyotolewa na taasisi hiyo Jumatatu wiki hii, rais huyo bora mstaafu wa Afrika atatangazwa mjini London, Uingereza na kamati ya Mo Ibrahim inayoundwa na watu saba waliowahi kuongoza taasisi za kimataifa.

Miongoni mwa wanakamati hao yumo Salim Ahmed Salim aliyewahi kuwa waziri mkuu na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ya Afrika (OAU).

Licha ya kiongozi huyo kutunukiwa fedha hizo taslimu, taarifa hiyo inaeleza kwamba maisha yake yote atakuwa akipewa dola 200,000 za Kimarekani (sawa na takriban Shmilioni 260,000 za Kitanzania).

Kiongozi huyo atakuwa ni wa tatu kutunukiwa tuzo hiyo Barani Afrika tangu taasisi hiyo ilipoundwa mwaka 2007.

Waliotunukiwa tuzo hiyo ni rais wa zamani wa Msumbiji, Joaquim Chissano aliyetunukiwa mwaka 2008 na Festus Mogae wa Bostwana (2007).

Mwaka jana kamati hiyo, iliyo chini ya katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, haikumpata mshindi wa tuzo hiyo.

Taasisi hiyo inaongozwa na mfanyabiashara tajiri wa Sudan, Mo Ibrahim, ambaye amebuni tuzo hiyo kwa lengo la kuimarisha demokrasia na utawala bora Barani Afrika.

Story na Leon Bahati
Source:http://mwananchi.co.tz
Jumatano, 26 May 2010 08:48

Makamba awangurumia makatibu uwenezi CCM

Katibu Mkuu wa CCM Yusuph Makamba, akionyesha vitabu mbalimbali vya maarifa na katiba ya chama mjini Dodoma, Jumanne wiki hii wakati wa ufunguzi wa semina kwa makatibu uwenezi wa CCM kutoka mikoa yote NCHINI. Kulia ni Katibu wa Itikadi na uenezi CCM Kepteni Mstaafu John Chilighati. Picha kwa hisani ya Israel Mgusi... Soma story hapo chini.....

Makamba atamba, aonya makatibu
Jumatano, 26 Mei 2010 08:47

Habel Chidawali, Dodoma

KATIBU mkuu wa CCM, Yusufu Makamba amewaonya makatibu wa siasa na waenezi wa chama hicho, akiwataka kutonunuliwa na wagombea ubunge na akajinasibu kuwa yeye ni mtu anayekwenda na wakati hivyo hawezi kung’olewa katika nafasi hiyo.

Makamba alitoa onyo hilo jana kwenye ukumbi wa NEC Mjini hapa wakati akifungua semina ya siku tatu kwa makatibu hao ambayo itamalizika kesho.

Makamba, ambaye anajulikana kwa ucheshi, pia aliwasimamisha kwenye mkutano huo baadhi ya viongozi wa jumuiya ya wazazi wa mikoa ya Tanga, Morogoro na Dar es salaam, akiwatuhumu kuwa ni vibaraka wa wagombea ubunge.

Katika hotuba yake, Makamba alitamba kuwa njia itakayomuokoa yeye asing’oke katika nafasi yake ni uamuzi wake wa kusoma kwa bidii.

“Mimi nimesoma na ninasoma kila wakati ndiyo maana sibabaiki kabisa... hata ukiniuliza jambo lolote naweza kukuambia kutokana na ukweli kuwa ninakwenda na wakati na nitaendelea kuwa hivyo kila mara ndio maana watu wanasema kuwa ning’atuke, lakini wanaishia kutokuwa na majibu kwa kuwa ninaenda na wakati," alitamba Makamba ambaye watu walitaka aondolewe baada ya CCM kuanguka kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime.

Aliwataka Makatibu hao kutumia muda wote wa kazi zao katika kupitia vitabu mbalimbali vikiwemo vitabu na vijarida vilivyoandikwa mambo ya CCM ili kujiimarisha katika misingi mizuri ya kupambana na maswali yanayotoka upande wa wapinzani.

Makamba, ambaye amekuwa akimnadi Rais Jakaya Kikwete kuwa ndiye mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama hicho, aliwataka viongozi hao kutokuwa vibaraka wa wagombea ubunge.

Kuhusu uchaguzi mkuu ujao, mtendaji huyo mkuu wa chama tawala alisema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni "ushindi ni lazima ndani ya CCM" na kwamba hilo lazima itekelezwe chini ya usimamizi wa makatibu hao.

“Kwa hiyo mkiondoka hapa msiende kulala; hakikisheni chama kinashinda kweli maana hata tafiti mbalimbali zilizofanywa zimeonyesha kuwa CCM inakubalika kwa asimilia kubwa,” alisema Makamba.

Alisema kuwa mbali na utafiti ambao umeonyesha kuwa Kikwete anakubarika kwa asilimia 85.5, uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana ulikuwa ni kipimo tosha cha kuonyesha kuwa CCM inakubalika baada ya kushinda kwa asilimia 91.7.

Source:http://mwananchi.co.tz

S

Hii ngoma itakuwa kama ya Liyumba au..????

Watuhumiwa wa kesi ya matumizi mabaya ya madaraka katika Serikali ya awamu ya tatu,kutoka kushoto Basil Mramba, Daniel Yona na Grey Mgonja, wakijadili jambo wakati wakiwa katika chumba cha Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam Jumanne wiki hii, wakisubiri kusikilizwa kwa kesi yao.Picha kwa hisani ya Michael Matemanga

JK ahutubia bunge Afrika Mashariki

Mwenyekiti wa jumuiya Ya Afrika Mashariki, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia bunge la jumuiya hiyo jijini Nairobi Jumanne wiki hii.Kushoto ni Spika wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mheshimiwa Abdirahin Abdi.
Rais Jakaya Kikwete (Katikati) akiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdirahin Abdi (kushoto) pamoja na Spika wa Bunge la Kenya Kenneth Marende(kulia) wakiwa katika viwanja vya Bunge la Kenya Muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili na kupigiwa wimbo wa taifa.

Rais Mwai Kibaki wa Kenya akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Nairobi jJumanne wiki hii kwa mazungumzo mafupi muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kulihutubia bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Picha zote kwa hisani ya Ikulu

Tuesday, May 25, 2010

Tanesco yapata bosi mpya

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imemteuwa Mhandisi William Geofrey Mhando kuwa Mkurugenzi mpya wa TANESCO. Uteuzi huo unaanza rasmi Juni 1, 2010.

Taarifa iliyotolewa jana (Jumanne) na Idara ya Mawasiliano ya Tanesco imeeleza kuwa Kabla ya uteuzi huo, Mhando alikuwa ni Meneja Mkuu Usambazaji umeme na Masoko katika shirika hilo.

Mhando anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika hilo, Dr. Idris Rashid ambaye muda wake wa uongozi katika shirika hilo umemalizika.

Mhando aliajiriwa na TANESCO October 1987 kama Mhandisi wa umeme, ambapo baadaye alipandishwa na kuwa Mhandisi katika line za umeme.

Mwaka 1990 hadi 1992 aliteuliwa kuwa Meneja wa TANESCO mkoa wa Singida ambapo baadaye mwaka 1992 hadi 1994 alikuwa Meneja wa mkoa wa TANESCO mkoa wa Mbeya.

Vilevile alipandishwa cheo mwaka 1995 na kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Kusini Magharibi hadi mwaka 1999.

Aidha, Mhandisi Mhando ana elimu ya Shahada ya Uzamili (Masters) katika masuala ya umeme aliyoipata Havana Cuba mwaka 1987, vile vile ana elimu aliyoipata katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Gari ya JK yabuma wakati wa msafara

Cruiser zilizokuwa zimembeba JK wakati wa ziara yake jumatatu jijini Dar zilibuma maeneo ya BP, Kilwa road(pichani juu) na maeneo ya Kimara, Morogoro road(pichani chini)... (picha kwa hisani ya mdau Michael Jamson)....soma habari zaidi hapo chini......
Gari la JK lazima ghafla barabarani
Tuesday, 25 May 2010 09:33
ZIARA ya Rais Jakaya Kikwete aliyoifanya jana mkoani Dar es Salaam ilipata mushkeli baada ya gari alilotumia kwenye msafara wake kuzimika ghafla mara mbili barabarani.

Gari hilo lilizimika kwa mara ya kwanza katika makutano ya barabara ya Morogoro na Mavurunza wilayani Kinondoni eneo la Kimara Mwisho majira ya saa 7:30 mchana ambako msafara wake ulisimama kwa dakika tatu.

Gari hilo lilizimika tena kama hatua 150 tu kutoka katika makutano hayo na ndipo rais akahamishiwa kwenye gari lingine lililokuwa kwenye msafara huo huku akiwa ananyeshewa mvua.

Tena majira ya saa 10:00 jioni msafara wake uliokuwa ukitokea Keko Toroli wilayani Temeke, ulikwama tena maeneo ya BP barabara ya Kilwa ambako gari hilo jipya nalo lilizimika ghafla.

Tukio hilo la kihistoria nchini, liliwapa wakati mgumu maafisa usalama ambao kila mara gari lilipokuwa limezimika, walishuka kwenye magari yao na kuondoa bendera na ngao.

Kusimama gafla kwa msafara wake eneo la Kimara, kulimlazimisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya kukimbilia eneo alilokuwapo rais huku umati wa watu uliokuwa umejibanza pembeni mwa barabara nao ukisogea karibu.

Ilimchukua takriban dakika mbili kwa maafisa wa usalama wa taifa kupata suluhu ya namna msafara huo utakavyoendelea kutokana na mkanganyiko wa gari ipi kati ya mbili zilizokuwa zinafanana aiangie rais.

Msafara huo uliendelea baada ya Rais Kikwete ambaye alikuwa amevaa shati la kitenge la mikono mirefu na akiwa analowa hasa miguuni kuhamishiwa katika gari jingine huku lile lililoharibika likiwa linasukumwa na umati wa watu hadi pembezoni mwa barabara.

Hata hivyo, baada ya dakika nane gari hilo aina ya Toyota Landcruiser VX V8 lililokuwa na rangi nyeusi, liliwaka baada ya dereva kujaribu kuliwasha kwa zaidi ya mara nne.

Kuzimika kwa gari lake eneo la PB kulifanya msafara wa rais usimame kwa takriban dakika kumi kabla ya kuendelea hadi Ikulu ambako alipumzika kwa muda na kuenda ukumbi wa Karimjee kufanya majumuisho ya ziara yake.
Source: http://mwananchi.co.tz

Monday, May 24, 2010

Hukumu ya Liyumba

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania-BOT Amatus Liyumba akipanda basi la magereza tayari kuelekea lupango kutumikia hukumu ya miaka miwili jela baada ya mahakama ya hakimu mkazi kisutu kumpata na hatia ya kutumia vibaya madaraka yake.
Hapa wandugu, jamaa na marafiki wakisikitika baada ya hukumu .........

Liyumba akishauriana na jopo la mawakili wa upande wa utetezi mara baada ya hukumu kutolewa......
Liyumba aki-'riakt' baada ya hukumu kutolewa.....

Hapa ni wakati alipowasili kisutu....... maphotoo kwa hisani ya wadau Fidelis Felix na Venance Nestory......

Vifaru warejea bongo

Baadhi ya maafisa ya shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) na wawakilishi wa mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali ambayo yanajihusisha na masuala ya uhifadhi, wakiwa wanapokea wanyama aina ya faru toka nchini Afrika ya kusini, jumla ya faru 6 kati ya 32 waliwasili mwishoni mwa wiki katika uwanja wa ndege wa Serengeti. Picha hii kwa hisani ya mdau Mussa Juma

Shule Girini eka yawaka moto

Baadhi ya wandugu wakiangalia majengo ya shule ya 'girini eka' yaliyochomeka.....
Hivi... hii hali inatokana na mgogoro ule wa wanafunzi na uongozi wa shule au ni viboko walivyochapwa madeni....? maswali mengi kuliko majibu...!!