Tuesday, November 15, 2011

MVUA YALETA DHAHAMA UWANJA WA NDEGE MWANZA

Ndege ya Shirika la PrecisionAir ikiwa katika maji katika uwanja wa Ndege wa Mwanza ambao ulijaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha jana (Jumatatu).
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika uwanja wa Ndege wa Mwanza hiyo jana (Jumatatu) baada ya mvua kuleta dhahama. 
Uwanja wa Ndege wa Mwanza ukiwa umejaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha. Uwanja huo ulifungwa kwa takriban saa sita. Kiasi cha Abiria wapatao 200 waliathirika na hali hiyo. Picha/ RAY NALUYAGA

LEMA APATA DHAMANA

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akitoka mahakamani baada ya kupata dhamana jana (Jumatatu). Mbunge huyo alikaa rumande kwa takriban siku 14 baada ya kukataa dhamana ikiwa ni njia ya kuonyesha kutoridhishwa kwake na vitendo vya vyombo vya dola kumuandama. PICHA/  FILBERT RWEYEMAMU

ZOEZI LA KUONDOA KWA NGUVU WAKAZI ENEO LA MAKAO, WILAYANI MEATU, SHINYANGA


Moja kati ya familia zilizoondolewa kwa nguvu katika eneo la hifadhi (Wildlife Management Area) lililopo eneo la Makao Wilayani Meatu Mkoani Shinyanga. Eneo hilo hutumika kwa shughuli za kitalii na uwindaji. 
Moja ya nyumba zinazodaiwa kuchomwa moto katika zoezi la kuondoa kwa nguvu wakazi katika eneo hilo. Takriban kaya 625 zinadaiwa kuishi katika eneo hilo. Picha / Zulfa Mfinanga

Sunday, November 6, 2011

Prince of Wales and the Dutches of Cornwell in Tanzania for a four-day official visit

 Askari akiwa katika doria JNIA 
 Mapaparazi wakisubiria ujio wa Prince Charles na Mkewe Camilla
 Ngoma ziliendelea kutumbuiza
 Ndege iliyombeba Prince Charles and Mkewe Camilla akigusa ardhi ya Tanzania tabrikan saa 12:15 jioni (6:15PM)/ 16:15HRS) Jumapili. Hii ni safari ya pili kwa Prince Charles kutembelea Tanzania tangu alipozulu nchini Machi 1984  

 Mmoja wa Marubani akihakikisha kama ngazi imeshawekwa vyema kabla ya kufngua mlango wa ndege
 Prince Charles na Mkewe Camilla wakiteremka toka kwenye ndege
 Hapa wakiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiangalia tumbuizo toka kwa vikundi vya ngoma za asili
Ziara hii ya siku nne inafuatia mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete aliotutoa kwa Prince Charles. Picha kwa hisani ya Fidelis Felix

Mahafali ya Nne ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE)




Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Kwanza katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa mahafali ya Nne ya chuo hicho yaliyofanyika Jumamosi (Novemba 5) jijini Dar es Salaam ambapo wahitimu 786 walitunukiwa Shahada zao. Tangu mwaka 2005 chuo hicho kimeshatoa walimu 3,884 wenye Shahada ya Kwanza.