Tuesday, April 9, 2013

MAGEREZA DODOMA WAKABIDHIWA MAGARI YA KISASA YA KUSAFIRISHA MAHABUSU KWENDA NA KURUDI TOKA MAHAKAMANI

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mabasi mawili na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Katika hotuba yake mkuu wa jeshi hilo aliwataka maofisa magereza wa mkoa huo wawe makini kuyatunza magari hayo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Dodoma Jumanne

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akikata utepe kuzindua rasmi jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mary Shangali, kushoto ni Mkurugenzi wa Mashitaka nchini(DPP), Dk.Eliezer Feleshi ambao walikuwa katika uzinduzi huo uliofanyika katika Gereza Kuu Isanga Dodoma Jumanne

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akiwasha moja ya magari yaliyozinduliwa kuashiria uzinduzi wa kuwasafirishia Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Isanga Dodoma Jumanne.

Magari matatu ya kuwasafirisha Mahabusu yaliyozinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, katika hafla iliyofanyika Gereza Kuu Isanga Dodoma Jumanne. Picha zote na Felix Mwagara.

No comments: