Tuesday, January 6, 2009

Habari zilizovunjika......Viongozi wa UWT Manyara wapata ajali......

Katibu Mkuu wa UWT mkoa wa Manyara, Verosa Mjema (chini) na Katibu muktasi wake Riziki Rashid Chikoko (juu) wakiwa katika chumba cha wagonjwa mahutuki katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kupata ajali ya gari katika eneo la chenene, Haneti wilayani Kondoa wakiwa njiani kuja Dodoma katika mkutano mkuu wa jumuiya hiyo. Kwa mujibu wa madaktari, wote wawili wamepata majereha makubwa kichwani na wanatarajiwa leo januari 07 kupelekwa muhimbili kwa matibabu zaidi. Blog hii ya wana idodomya inawatakia ugua pole viongozi hao wa uwt mkoa wa manyara... mwenyezi mungu awajalie wapate pona mapema na kurejea katika ujenzi wa Taifa….



Katibu Mkuu wa UWT Mkoa wa Manyara Verosa Mjema pamoja na katibu muktasi wake Riziki Rashid Chikoko wamejeruhiwa vibaya baada ya kupata ajali ya gari katika eneo la chenene, Haneti wilayani Kondoa jana Januari 06 wakiwa njiani kuja Dodoma kuhudhuria mkutano mkuu wa jumuiya hiyo unaoanza leo Januari 07.


Kwa mujibu wa madaktari katika hsopitali hiyo, Verosa na Riziki wamepata majeraha makubwa kichwani ikiwa ni pamoja na mipasuko wakati riziki ameumia pia jicho lake la kushoto.


Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Jacob Chembele amesema majeruhi hao wanatarajiwa leo Januari 07 kusafirishwa kupelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa Matibabu zaidi.


Jumla ya watu watano wamejeruhiwa katika ajali hiyo ya gali iliyokuwa na watu sita wakiwahi mkutano huo.


Miongoni mwa wailojeruhiwa ni pamoja Suzan Maliki aliyeumia jicho la kushoto kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo ya mkoa, Phillemon Saigodi.

Wengine ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Manyara Elizabeth Malle na Christina Simon aliyepata majeraha madogo ambapo walitibiwa na kuruhusiwa.


Hata hivyo kwa mujibu wa Dkt. Saigodi mtu wa sita aliyetajwa kwa jina la Mama Chonjela aliyekuwa pamoja na majeruhi hao katika gari hiyo aina ya pajero hakufikishwa hospitali na haikufahamika mara moja iwapo alipata majeraha au laa.


Maandalizi wa UWT

Vijana wa CCM wakiweka bendera katika mtaa wa Kuu street ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM utakaoanza Jan 07. JK anatarajiwa kufungua mkutano huo ambao pia utafanyika na uchaguzi mkuu wa viongozi wa kitaifa wa jumuiya hiyo. Mchuano mkali unatarajiwa katika nafasi ya mwenyekiti ambapo wagombea watatu Janeth Kahama, Sophia Simba na Joyce Masunga.
Itakumbukwa mwaka jana vyombo vya habari viliripoti kutokea kwa purukushani za hapa na pale baina ya wagombea wawili wa nafasi hiyo. Yetu machu na masikio tusubirie kitakachojiri hapo kilimani club.....!!!!

Monday, January 5, 2009

BORA ATCL IONDOKANA NA HAYA....!!!

Bila huruma ya sirikali.... Any Time Canceled Limited ingewafika haya.....!!!

Dom Masterplan

Kwa wale wenye nia ya kuwekeza katika mji mkuu wa Tz....... hii ndio ramani ya jinsi mji utakavyokuwa... Ramani kwa hisani ya CDA

Lugha za watu bwana....!!!

Hii kibande imetoka kwa mdau Titus Nyange........

Haya Marimba yanahusiani nini na ICT??

Makamu wa Rais wa kampuni ya IBM, Dr. Mark Dean akiadmire marimba alopewa kama zawadi alipotembelea chuo kikuu cha dodoma-udom- recently.... pembeni yake ni VC Prof. Idris Kikula

Sunday, January 4, 2009

MZUNGU KWA NGWASUMA... UTAMTAKA BABAKE...!!!

ALIANZA HIVI......
IKAWA HIVI......
MZUKA UKAZIDI NAMNA HII......
ATATOA VITU ZAIDI KAMA HIVI......
AKAMALIZIA NAMNA HIII......

Survival for the fittest....!!!!

Ndo maisha yalivyo....hususan kwa wanyama wasio na utashi......... mbabe ndo anaendelea kula hewa ya hii dunia......!!! sio lazima iwe porini tu.... ata uraiani....!!!

Duu....si ungemgea na mwezio moja aride...?

tofauti na usafiri wa bush kantri.... dauntaun urahisi upo kiaina kwani mbali na mtuka na tukutuku kuna ngwinjo.... kama anavyonekana jamaa kwa picha.... ila mshkaji anaonekana mchoyo kichizi.... kwani angemgea ata mwingine aendeshe adi wanapoenda...... WATU KAMA HAWA WAKIWA NA GARI... UKIMWOMBA LIFTI UTASKIA..."MAFUTA HAYATOSHI WATU WAWILI...." huku sura kageuzia asipokuangalia....!!!1 tehe tehe tehe...!!!

Saturday, January 3, 2009

Usafiri wa vijijini....


Dogo akiride ng'ombe wanaovuta mkototeni akiwa kwa njia katika kijiji cha mpunguzi kwenda chukua mbolea.....Ukiwa nayo hii bush kwetu.... uko juuu vibaya mno....

Vichwa TRL kweli vimechoka....!!!! Kumbe ndo maana enz za mwl waliitaga gari moshi...!!!

Injini ya treni ikitoka stesheni ya dom njiani kuelekea bara..... kilichonivutia ni hali ya utoaji moshi mwingi mno..... hii ni moja kati ya uchafuzi wa hali ya hewa........!!!

Kiu sooo...!!!

Mgambo aliyekuwa akiangalia usalama wakati wa mkutano wa hadhara kijiji cha nmpunguzi kilichopo nje kidogo ya manispaa ya dodoma katika barabara iendayo kwa wanyalukolo alishindwa kuvumilia na kundaka mama mmoja ampe malenga ga kunywa..... alipokuwa akitoka kisimani....Kiu kweli noma..... ila bora huyo kiu cha maji.... wenzangu na mie mna viu vingi.... vingine ata sivitaji....!!!

Mnaokuja Dom muwe macho....!!!

Eneo la mlima uliyopo dodoma makulu ambapo alimanusura matapeli watatu wawili kutoka dsm wakiwa na mwenyeji wao wamlize babu wa watu kutoka rombo kiasi cha sh40m...fedha ambayo babu huyo aliipata baada ya kuuza nyumba yake iliyopo dsm.... hata hivyo polisi mkoani dom walistukia game na kumwokoa babu huyo asitapeliwe......
Eneo hili ndilo babu huyo toka rombo alipoambiwa kuwa atazungumza na babu anayeweza fanya mazingara chapaa hizo Sh40m zikawa Sh600m.....
Hapa kuna mishumaa pamoja na udi ambayo huwashwa na kumpumbaza mtapeliwa kuwa ataongea na maruhani.... ila kwa mbele kama anapoelekea kamanda mmoja pichani kuna tundu la kutokea upande wa pili.... ila kwa juu yake kuna madondora kichizi.....!!!

MGAMBO SHUGHULI......!!!

SIO KWAMBA VIJANA HAWATAKIJIUNGA MGAMBO.... ZANA NDUGUYANGU....!!!

Vijana hawa wamefuzu mafunzo ya mgomba.... wakimsikiliza mgeni rasmi.... ila chek buti za washakaji hao wabee.....!!!

KIGELEGELE......!!!

Mdala wa kigogo akitwangwa kigelegele....!!!!
kigelegele kingine hicho...si mchezo.!!!!

MAJUKUMU HAYA YA KIFAMILIA ADI NGOMANI....?!!!!

Hebu nishkie mwanangu.... mie nikacheze ngoma....!!!
Ebana kumbe unakatika kichizi.....!!!!
Hebu acheni utani..... hawa wana mtakaanao tu.... hadi tumalize kucheza ngoma....!!!
Ebana mzee mwezangu hawa wanawake ngangari kichizi.... ila poa tu.....kubeba mtoto kwa nini!!!

KINADADA WAVUMILIVU KWELI.....!!!

Ingawa hupenda sana kusuka mitindo ya nywele ambayo wasusi wake hutokea katika jamii za wamasaai, inavyoonyesha kinadadazetu huwa wavumilivu sana... kwani mbali na kukaa kitako muda mrefu.... kajismell ambacho hutoka kwa wasusi hao.. hususan katika mkao kama huu unaoonekana pichani.....mhnmmn... mie chichemi....!!!

MADEREVA BWANA.... NOMA KICHIZI....!!!!

Haya sasa.... huyu naye tena anamdraiv mheshimiwa... ila angalia alipoegesha gari.....!!!!
Huyu naye baada ya kumwaga mchanga.... tipa limekataa kurejea sehemu yake.... akaamua kutambaa hivyo hivyo.... huku deiwaka wake akiwa nyuma kimashakamashaka....!!!
Mwingine kaamua tu kudharau ishara ya barabarani (kushoto) inayomwonyesha kuwa hiyo ni njia moja tu.... hairuhusu gari kuenda upande anaoelelea...........!!!!

ARE THESE GENDER ISSUES OR SEX INDIFFERENCIES....?!!!!

jAMANI HAPA TUNAKADIBEIT KAKIAINA..... HUSUSAN KWA UPANDE WA ADAMA HAWA JAMAA ZETU AKINA HAWA WAMEKUWA WAKILAUMU SANA KUHUSU KUACHIWA MZIGO WA MAJUKUMU KAMA VILE PICHA INAVYOONYESHA MAMSAP KABEBA ZIGO LA KUNI HUKU MZEE MWENZANGU AKIWA NA KIDUMU, JEMBE NA KAMFUKO KENYE NYANYA... AMBAPO WAKIFIKA HOME... MZEE MZIMA ATAKUNJA NNE HUKU MAMSAP AKIINGIA KWA JIKO KUREKEBISHA MENYU....!!! HEBU SOMA HAKO KAFUNGU KA MISTARI HAPO CHINI .... AFU DISAID MWENYEWE KWA MKICHWA......



ARE THESE GENDER ISSUES OR SEX INDIFFERENCIES....?!!!!
If you work too hard, there is never any time for her.
If you don't work enough, you're a good-for-nothing bum.

If she has a boring repetitive job with low pay, it's exploitation.
If you have a boring repetitive job with low pay, you should get off your butt and find something better.

If you get a promotion ahead of her, it's favoritism.
If she gets a job ahead of you, it's equal opportunity.

If you mention how nice she looks, it's sexual harassment.
If you keep quiet, it's male indifference.

If you cry, you're a wimp.
If you don't, you're insensitive.

If you make a decision without consulting her, you're a chauvinist.
If she makes a decision without consulting you, she's a liberated woman.

If you ask her to do something she doesn't enjoy, that’s domination. If she asks you, it's a favor.

If you try to keep yourself in shape, you're vain.
If you don't, you're a slob.

If you buy her flowers, you're after something.
If you don't, you're not thoughtful.

If you're proud of your achievements, you're an egotist.
If you're not, you're not ambitious.

If she has a headache, she's tired.
If you have a headache, you don't love her anymore.

Mambo ya Kumnadi...... Msalaatoooo...!!!!

jamaa akiweka vyema zagazaga mahususi... kwa mtafuno... maeneo ya kumnadi jirani tu kwa kwa mzee wa sumo... msalaatooo nje kidogo ya dom manisipo...... huko ni maarufu sana kwa bia choma na nyama.... kwa bei nafuuu...!!! kilo buku 4 tu....!!!
ila kinachowaliza hawa jamaa zangu ni kwamba machinjio holela kama ya huko kwenye kumnadi yamepigwa marufuku...kutokana na hijenik poposez...... sasa kuwalazimu wachinje katika machinjo ya kisasa yaliyopo kizootaa...!! wenzangu na mimi wasio na ubovu wa meno wanatia shaka juu ya kupanda kwa nauli ya nyama...... itakuwa sasa ikiuzwa zaidi ya buku 4 za sasa... yetu majicho wacha tusubiri tuone......

Hizi ngoma zilipigwa live... bila chenga....!!!!

Mjeda akikusanya njugu zilizotawanyika baada ya kutoka katika binduki....!!!
ziliwakuwa nyingi...... ila ushahidi lazima uishe.......usibaki ata chembe!!!
Hili la machozi halikulipuka....... watanganyika wakaliokota....!!!!
Mengine yaliyolipuka haya hapa.........!!!

TBT/KIMANGA-MWENGE hadi DOM

Daladala lenye TLB ya T/Kimanga-Mwenge jijini Dsm likila vicha mjini Dodoma karibu na stendi kuu ya mabasi yeendayo mikoani.......!!! Kweli eniwea...!!!

Mwaka mupya na lebal mpya

Wakazi wakisherehekea na bia bora yenye ladha saaaafi....!!!!

Thursday, January 1, 2009

Kumbe hii ndio bahi….!!

Mbuzi aliyekuwa akila ride juu ya kichwa cha scania akiangalia mandhari ya bahi wakati lori hilo lililokuwa safarini liliposimama kwa muda maeneo hayo …..

Punda TZ dili...!!!

Huyu Mwaha mkazi wa eneo la maili bee mjini idodomya akiswaga punda wake wakirejea kukaya baada ya kusaka wateja wa mkaa ambao amembebesha punda huyo. Baada ya kulonga nae kiaina nikiulizia iwapo anaweza kuuza punda huyo, hakusita kunipa bei ya kilo moja unusu...!!!



Tuesday, December 30, 2008

Salaam toka idodomya...!!!!

Ndugu zangu wa damu mdumu...!!! kwanza babisa awali ya yote na kazalka, napenda kuchukua fursa hii, kusimama kidete hata kukaa kitako, kuwashukuri ninyi nyote mablogger na watalii wa blog kwa kuendelea kutoa motisha kwa pande zote mbili kuendelea kupost majamboz kwa blog zao kuweza kuwashawishi mzitembelee......!!!

Nawatakia kheri ya mwaka mupya 2009, ili uwe wa mafanikio kwa kila mmoja wetu..... !!!