Tuesday, March 16, 2010

Siku ya wanawake....

Wakinamama wakimsaidia msichana ambaye alizidiwa wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa mjini Dodoma hivi karibuni.... Mwanamana akiwa na watoto wake wa kike wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa mjini Dodoma.......

Mwanamke na Maendeleo

Mwanadada akizunguka katika mitaa ya mji wa Dodoma akitafuta wateja wa karanga huku akiwa na mwanae mgongoni......Ni Kweli "mwanamke na maendeleo tufanye kazi tusonge mbelee......"??

Mbinu mpya ua ukulima wa Zabibu

Mtaalam wa Kilimo cha Zabibu kutoka Afrika Kusini Dirk Bosman akionyesha mbinu mpya za ukulimwa wa zabibu wakati wa ziara ya mafunzo kwa wakulima wa zabibu katika kijiji cha Mpunguzi mjini Dodoma hivi karibuni. Kwa mbinu hizi mpya, mkuliwa anaweza kuvuna tani kati ya nane hadi 13 kwa ekari ikilinganishwa na tani za sasa tatu hadi tano kwa ekari...... Meneja Mkuu wa Kampuni ya Vinjwaji vikali vya Tanzania Distillers Limited (TDL) akiangalia zabibu zinazolimwa mkoani Dodoma. TDL inampango wa kufufua ao la zabibu mkoani Dodoma ambao hutoa takriban hectolitres 120,000 za malighafi inayotengenezewa Wine aina ya Overmeer pamoja na kinywaji kikali aina ya Value.....

Maadhimisho Wiki ya Nssf yaanza

Wanachama wa shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) wakipata huduma katika ofisi ya mkoa wa Dodoma ikiwa sehemu ya ni maadhimisho ya wiki ya shirika hilo nchini kote.
Ngoja nikuandikishe ndugu...... uchukue kadi yako.....nawe uwe mwanachama....

Glaukoma yaleta upofu kimya kimya.....

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, John Tupa akimvisha miwani Kaundime Seleman wakati wa maadhimisho ya kimkoa ya siku ya Glaukoma Duniani mjini Dodoma hivi karibuni. Mkoani Dodoma pekee takriban watu kati ya 10,000 na 12,000 wamebainika kuugua ugonjwa huo ambapo kati ya hao wagonjwa kati ya 1,500 na 2,000 wamepata upofu kutokana na glaukoma.
Hapa Mkuu huyo wa Wilaya akipimwa uwezo wa jicho kuona taswira na mtaalam wa tiba za macho wakati wa maadhimisho hayo.....

Saturday, February 20, 2010

Wajeda na mavituz yao

Huyo jamaa mkufunzi wa makaratee...yuko fit kinoma.... hapa kanivunjia nazi kwa ngumi... si mchezoo.... niliikagua nazi hiyo kuona kama ilikuwa na ufa kabla ya kupasuliwa.... sikuona kitu....
Wazee wakivuka vikwazo mbali mbali....








Si mchezo babake......




Hawa jamaa wako fiti kinoma

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi wakioyesha umahiri wa Karate wakati wa gwaride maalum la kufunga mafunzo ya kozi ndefu katika Kambi ya Jeshi ya Makutupora mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Jumla ya wahitimu 549 wakiwemo wanawake 86 wamefuzu mafunzo hayo Endelea kuangalia upate uhondo....
Hapa mambo ya kujihami kwa singe.....huyo hapo ni binti..... naye yuko fit kinoma...

Wajeda wakila kiapo cha utii na uaminifu.....



Shingo kulia.... saluti


Mkuu wa Utendaji Kivita Jeshini Brigedia Jenerali Farah Abdi Mohamed akikagua gwaride maalum la vijana wake......

Monday, February 8, 2010

Air Zara Ikitua jana

Ndege ya shirika la Ndege ya Air Zara ikigusa ardhi ya mji wa Dodoma kuashiria kuzindua safari za ndege hiyo mjini Dom.

Taa kushneh....Uzembe wa madereva

Daladala ikipita karibu na taa ya barabarani iliyopo katika barabara ya Dar es Salaam mjini Dodoma iliyogongwa na gari ambalo halijafahamika mwishoni mwa wiki... si unajua tena kipindi hicho madereva wengi wanakuwa ke..kee..rorooo... Ajali nyingi za nanma hii zimeelezwa kuwa zinazokana na uzembe

Air Zara yazindua safari Dom

Ndege ya Air Zara International aina ya Embrear 120 yenye uwezo wa kubeba abiria 30 ikiwasilis katika uwanja wa ndege wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa safari zake. Imeelezwa kuwa uwanja huu umekosa huduma za usafiri ..ati wenyewe wanaziita commercial flights... tangu mwaka 2000.
Waziri wa Miundombinu Dr. Shukuru Kawambwa akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Air Zara International, Misha Mango (kushoto)baada ya uzinduzi wa safari za ndege za shirika hizo kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma

Waziri wa Miundombinu Dr. Shukuru Kawambwa akishuka toka katika Ndege la Air Zara International Ndege aina ya Embraer 120 katika uwanja wa ndege mjini Dodoma

Rubani wa Shirika la Ndege la Air Zara International, Jaco De Vries akimuelezea Waziri wa Miundombinu Dr. Shukuru Kawambwa (kushoto) kuhusu mbinu za kurusha ndege

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Air Zara International, Misha Mango akimuelezea Waziri wa Miundombinu Dr. Shukuru Kawambwa (kushoto) kuhusu safari za ndege za shirika hilo

Wabunge wa Uganda wakizimia Chuo Kikuu Dom

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya bunge ya bajeti ya bunge la Uganda wakimsikiliza makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati walipotembelea chuo hicho hivi karibuni. Hapa wakiwa katika ka-tour kuzunguka chuo hicho kwa basi kwenye barabara ya jumla ya urefu wa kilometa 35 kuzunguka chuo hicho.
Makamu Mkuu wa UDOM akiwapa maelelezo wabunge hao ofisini kwake.

Waheshimiwa hawa kutoka Ugnada wamekubali juhudi hizo... walikuwa wakijiuliza mbona kwao wamelala mnoo.....

Siku ya Kupiga Vita Ukeketaji

Baadhi ya wanaharakati wa kupinga ukeketaji wakiwa katika maandamano kuadhimisha siku ya kupinga Ukeketaji Duniani iliyofanyika kitaifa mjini Dodoma.
Imeelezwa kwamba ingawa hakuna takwimu rasnmi za kitaifa za hivi karibuni, ukeketaji nchini umepungua kwa ujumla toka asilimia 18 mwaka 2002 hadi asilimia 15 mwaka 2008. Mkoa wa Manyara ndio unaoongoza kwa kuwa na asilimia 54 ya vitendo vya ukeketaji.

Madenti wa shule za msingi katika manispaa ya Dodoma nao walikuwemo...

Thursday, December 31, 2009

Ni kutokujua kusoma au ukaidi...?


Mfanyabiashara ndogondogo akiuza ndizi katika eneo linalokatazwa kandokando ya barabara ya kuelekea hospitali kuu ya Mkoa wa Dodoma. Lakini kwa nyuma askari nao wakipita na hamsini zao, ingawa bango linalokataza biashara limeandikwa kuwa na amri halali..... Hapo sasa....

Monday, December 14, 2009

Usafiri Wilayani....

Usafiri maeneo ya wilaani si mchezo .... kama unavyoshughudia hapo katika picha nilizonasa kwenye barabara ya Dodoma-Kondoa..... hiyo land-rover 110 imejaza mizigo kupita kiasi huku jamaa wakiwa wanakula upepo juu..... hapa chini ni basi aina ya isuzu journey ..... tingo katoka juu kurekebisha mizigo wakati gari ipo katika mwendo... akabidi aingilie kwa dirishani...

Sunday, December 13, 2009

Ndani ya Dom: Str8Muzik Festival:InterCollege Special 2009

Waliofanya ridhim ziende vyema vilikuwa hivi vichwa...Ma-DJz hawa wakiwa kwa kazi.......
Hip Hop artist toka Kenya..... Nonini... al-mahruf kama..Genge.... akichana Keroooro.....

Wazee wa Keroro nao kwa floor wanazidi pagawa.......


Msaanii huyo nae .....Amani Swazagone... alikonga nyoyo za madent.... hapo royal village mjini Dom......

Izo Bizzness na Quick Racker wakifanya mambo kwa stage...... ebana si matani kilele cha Str8Muzik Festival:InterCollege Special 2009 ....'kilinoga kunoga.......'

Str8Muzik Festival;Intercollege Special 2009

Joe Makini a.k.a Mwamba wa Kaskaz.. akimwaga mistari wakati wa music bash.... Str8Muzik Festival:InterCollege Special katika hotel ya Royal Village mjini Dodoma usiku wa Jumamosi (Dec 12) kuamkia J'2 (Dec 13).
Mzee wa Shikide... Dully Sykes a.k.a Mr. Misifa akibembea na 'bamutu bataokota benyewe kunyavu.....'

Crowd ilikuwa hot... ukizingatia madent wa colleges za Dom... plus kilauri.... ilikuwa balaa......

Albert Mangwair....mwana wa East Zoo.... akiwaambia 'nipeni..nipeni deal masela.... nikamate mahela...'

Ndo hapo alipowachanganya wana East Zoo........

Sunday, October 18, 2009

Moh Trans yapata ajali

Abiria wakishuka kutoka katika basi la Mohammed Trans lenye namba za usajili T779 AWH katika kituo cha Mabasi Mjini Dodoma Jumatano (14/10/2009) usiku. Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma lilipata ajali baada ya kugonga lori katikati ya eneo la Gairo na Pandambili ambapo mtu mmoja alikufa papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Tuesday, October 13, 2009

Mwanamke Anayetoa Machozi ya Damu Kila Anapolia

Rashida Khatoon Sunday, April 19, 2009 4:12 AM
Mwanamke mmoja nchini India amejipatia umaarufu na kuwa gumzo nchi nzima kutokana na hali yake ya kutoa machozi ya damu kila anapolia. Rashida Khatoon mkazi wa mji mmoja kaskazini mwa India, amewashangaza hata madaktari kwa hali yake hiyo ya kutiririka machozi ya damu kila anapolia.

Kwa siku mwanamke huyo humwaga chozi la damu mara kadhaa.

"Sisikii maumivu yoyote, badala ya machozi ya kawaida, damu zinapotitirika ni kitu cha kushangaza" alisema mwanamke huyo ambaye amekuwa gumzo sana nchini India.

Viongozi wa dini wa India wanadai kwamba mwanamke huyo ni miujiza toka mungu.

Kutokana na umaarufu mkubwa aliojizolea mamia ya watu wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa mwanamke huyo kujishuhudia wenyewe kwa macho yao.

Wageni hao wamekuwa wakimmiminia mwanamke huyo na familia yake zawadi kadhaa kila wanapomtembelea nyumbani kwake.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetai...1790150&&Cat=7

Friday, August 28, 2009

Uzembe mwingine bwana... wee wacha tu...!!!

Gari ikiwa imetupwa kiasi cha mita 50 toka mahala ilipogongwa na kiberenge eneo la majengo mjini Dodoma hivi karibuni wakati dereva akitaka kuwahi kuvuka kabla ya kiberenge hicho kupita.
Baadhi ya mashuhuda wakiangalia gari hilo ambapo hata hivyo hakuna abiria aliyejeruhiwa saaana.....
Mmoja wa walioshughudia ajali hiyo akijaribu kuelezea ilivyotokea....si unajua jinsi tulivyo hodari katika kusimulia.... kama movie vile.....!!!