Thursday, August 4, 2011

Hii faini kwa smoking

Katika Jiji la Nairobi na miji mingine mikubwa nchini Kenya... uvutaji wa sigara hadharani na kwenye mikusanyiko ya watu pamoja na mitaani umepigwa marufuku... ukikamatwa tu ukivuta fegi... hiyo ndo adhabu yake.... kutokana na kuanzishwa kwa sheria hiyo..... maafisa watendaji wa  miji waliamriwa kutoa matangazo kwa umma kwa lugha ya kiswahili..... hapo ndimbo mbavu zinapovunjika.....nasikia wengine bado wanaandaa matangazo yao... hawajaweza maliza bado.... aliyepatia kidogo kiswahili ni wa mji wa Pwani.
The Coast Town Clerk:Uvutaji wa sigara umepigwa marufuku kuanzia leo.Watakaopatikana wakikiuka amri hii wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Nyote zingatieni.

The Kiambu Town Clerk:Wanyuanji wa thigara washunge sana . Unyuanji wa thigara bere ya watu hata huko ije umefigwa marufuku na kaju kuanjia reo.

The Machakos Town Clerk:Wavulutanji tusikala wasunge sana . Sasa kuvuluta tusikala ni maluvuku na kanzu ya Masaku itawasukulia atua kuvwa sana.

The Kisumu Town Clerk:Atenson Plis!!! Mifuto sgara adharani sasa omepigwa marofuku. Okipaatwa ibiro yie Kodiaga! Apana furuta Plis!!

Wajir Town Clerk:Habana iko buruta sigara. Yeye lishapigwa marufuk na sisi tagaamata mutu
bhahala yaghe kiburuta.


Kericho Town Clerk:Gutoga leo gugunywa na gufuruta sigara sisi nagshagataasa. Haguna!! Charipu wee taona!!!

Saturday, July 30, 2011

Mambo ya Nairobi...

Mdada shoe shiner akimhudumia mteja.....kwa bongo... hapo wavua viatu... wengine... hususan wakinababa... soksi huwa na hitilafu......

Wednesday, July 27, 2011

It is So Sad...!!!

Judge to child: Do you want to live with your mother?

Child: No

Judge: Why?

Child: She beats me.

Judge: Okay, so you want to live with dad?

Child: No

Judge: Why not?

Child: He beats me too.

Judge: So who do you want to live with?

Child: Taifa Stars.

Judge: WHY??

Child: They never beat anyone!

Lady on Bicycle Grabs Too Much Attention

I received this attachment kwa email... then found it worth to share na wadau..... just have a look... it is interesting....

Tuesday, July 26, 2011

South African 'corpse' wakes up

A 50-year-old South African man thought to be dead woke up in a chilly morgue on Sunday and shouted to be let out, scaring off two attendants who thought he was a ghost, local media reported.
"His family thought he had died," health spokesman Sizwe Kupelo told the Sapa news agency.
"The family called a private undertaker who took what they thought was a dead body to the morgue, but the man woke up inside the morgue on Sunday at 5:00 pm and screamed, demanding to be taken out of the cold place."
This caused two mortuary attendants on duty to flee the building in the small town of Libode in the rural Eastern Cape as they thought it was a ghost.
After calling for help and returning to find the man alive, an ambulance was sent to fetch the man who had "been exposed to extreme cold for nearly 24 hours" said Kupelo.
He said the public should not assume that a sick person had died and contact a mortuary, the report said.
"Doctors, emergency workers and the police are the only people who have a right to examine the patients and determine if they are dead or not."
Reported by Marco Longari | AFP – Sun, Jul 24, 2011

Monday, July 25, 2011

Kamanda Magufuli upo...? Wao waweze wana nini na sie tushindwe kwanini?

 Moja kati ya Fly-over nyingi zinazoendelea kujengwa jijini Nairobi... ikiwa ni jitihada za kupunguza msongamano barabarani..... Sasa sie wabongo sijue tume..gwa.... coz hadithi za fly over ni nyingi mno kuliko utekelezaji......Wao waweze wana nini na sie tushindwe kwanini?




Tempo....

 Nilivutiwa na hicho kifaa katika tempo moja jijini Nairobi... sijui tukiite gari... tolori ama nini??... kwa wale wanaojua tuelezeni kazi yake

Mambo ya Kispoti

 Jamaa akiranda mitaa ya jiji la Nairobi... na ka-sports......
Ila ukiwa bongo... na juu lilivyo kali na vyua sizizoeleweka soo kichizi...

Marikiti..Kisutu yao

 Soko la Ngara jijini Nairobi maarufu kwa matunda na mboga za majani.... kwa wakazi wa Saridalama.. ni kama vile la Kisutu... wadosi ndo kwao....



Sunday, July 24, 2011

RIP Bro Danny Mwakiteleko

Kwa kweli it is so sad.... sometimes unaweza sema God is not fair... but that is how it is...tulikaa nae tarehe July 3 usiku pamoja na Bukuku na jamaa wengine wawili... hii ndo ilikuwa last time nimeiona sura ya Danny......inasikitisha lakini hatuna jinsi.... nimejaribu kuangalia katika facebook... jinsi jamaa na marafiki walivyoguswa na msiba huu...rest in peace Bro...


Mpoki Bukuku: they say danny is no longer, sitaki kuamini! inauma sana!
Geoffrey Ng'humba: Saa ngapi sasa alipofariki? maana taarifa za magazeti ya asubuhi zimesema alitembelewa na rais na kwamba hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri? Oooh God! R.I.P. Danny.
Tausi Mbowe: bukuku inauma ndugu yangu sitaki kuamini kama Chifu Danny niliyemfahamu since 2001 sasa hatunaye, ndio hivyo tumuombee tu Mungu amlaze pema peponi kwani mbele yake nyuma yetu
Reginald Miruko: Kwaheri Kamanda Danny Mwakiteleko. Umetangulia kutuandalia makazi. Tulikupenda sana, lakini Mungu amekupenda zaidi. Ulikuwa kioo kwenye taaluma ya habari, tumejifunza mengi kutokana na ujuzi wako. Kifo chako kiwe chachu ya kupambazo na ajali za barabarani zinazoongezeka kila kukicha. Poleni wanahabari, wahariri, familia ya Mwakiteleko, ndugu na marafiki. Mungu ametoa, Mungu ametaa, jina lake lihimidiwe.
Teddy Mapunda RIP Danny Mwakiteleko 'You’ll be missed by SBL Team and will bring tears to everyone. It’s terrible when a person’s life becomes shorten by the quickest moments with so much to live for. You have brought happiness and joy to many people, for that is a true blessing for one to live for. R.I.P Danny
Teddy Mapunda Yes it is indeed! We were together in Arusha Moshi less than a week ago during editors Forum! This is the reminder from Allah that life is too short and we need to love each other and celebrate life together
Cecilia Mhina Ooh! Poleni sana jamani miaka ya mwanadamu duniani si mingi, Mungu huchuma ua lake wakati wowote apendao Mungu ailaze Roho ya Danny mahali pema Amen!
Moshi Goodluck Poleni sana familia ya Danny Mwakiteleko na wafanyakazi wa New Habari (2006) Ltd ,ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito.I will really miss his news from RAI magazine.Rest in Erternal peace my friend Danny!!
Zena Chande Ndugu yangu, matonya aliimba dunia mapito, tuwaombeni waliokufa waende salama, mimi na wewe hatujui siku yetu lini, pumzika kwa amani kaka Danny 'Patna', siku moja tutakutana
Adam Fungamwango Poleni sana wote walioguswa na msiba huu ndugu jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzake na hata sisi wenyewe waandishi! Ni kweli amekwenda Danny inauma sana, itabaki historia yake!
Benjamin Thompson Ooooh God Ooooh God why call our brother Danny Mwakiteleko now the time when we need him most!!May you please rest his soul in your eternal peace
Lwaga Mwambande Kazi ya Mungu haina makosa. Tumkumbuke Danny kwa mema yote aliyoyatenda wakati alipokuwa pamoja nasi.
Sudi Mnette Kazi ya Mungu!!
Peter Mgongo Ni msiba mkubwa kwa familia na jamii ya wana habari kwa ujumla, poleni wanafamilia wa marehemu Danny mwakiteleko mungu
awafariji ni mipango yake

Mroki T Mroki Kuna picha nimeziweka bloguni kwangu unaweza lia. Nikama alikuwa akituaga kule Arusha last week.
Bernard Rwebangira Duhh! nimeisikia muda c mrefu, RIP Danny!
Leah Mwainyekule He will surely be missed. So, so, so, sad jamani. Mwee!
Neema Mbuja Jaman mimi kama mwanahabari nimesikitishwa sana jamani sisi tulikupenda mungu amempenda zaidi
Rose Athumani Hee Mroki, kweli!!!Mungu amlaze mahala pema peponi!!! Still can't believe it!!!!
Geoffrey Ng'humba Pia tumwombee mwenzetu ndg. Kulekana, Mhariri msanifu wa DAILY NEWS ambaye anaumwa na amelazwa katika hospitali ya H. H. Agakhan Dar es Salaam. Mungu amwondolee adhabu ya maumivu na amjalie uponyaji wa haraka, Amen.
Exuper Kachenje Mungu ndiye hakimu na daima kazi yake haina makosa, Danny kwangu alikuwa mwalimu, nakumbuka alivyoniongoza kujiamini katika kazi yangu na kuwa makini. Katika hilo nitamkumbuka daima. Yeye ametangulia na kila mmoja na njia yake, lililo kubwa ni kumwombea Mwenyezi Mungu ampokee katika nuru ya uso wake mtakatifu apumzike kwa amani, Amina!!
Ibrahim Bakari Dah! Kamanda ametoweka, alikuwa si mhariri tu, pia ni kiongozi kwa waandishi, alikuwa mwalimu, alikuwa mtu wa changamoto katika uandishi wa habari. Kilichobaki tufuate yake mazuri. Mungu akupe amani ya milele, Danny.
Joseph Zablon Wengi tuliopitia katika mikono yake hatukutoka tupu, kuna ujumbe aliuleta duniani, amemaliza kazi yake na sasa kaenda kupumzika. Mungu ailaze mahali Pema Peponi Amina.....
Simba Deogratias RIP Danny.

Friday, July 22, 2011

Muswada wa kuongeza muda wa kunywa pombe kenya

Wanywa vileo nchini Kenya watakuwa na kila sababu ya kufurahia iwapo bunge la nchi hiyo litapitisha muswada wa sheria unaolenga pamoja na mambo mengine kuongeza muda wa kufunguliwa kwa sehemu zinazouza vileo (baa) kutoka muda wa sasa wa saa 6 hadi kufikia saa 12 kwa siku.

Kwa sheria iliyopo sasa, baa hufunguliwa kuanzia saa 11 jioni na kufungwa saa tano usiku kwa siku za kazi (week days). Iwapo muswada huo utapita, inamaana kuwa baa zitafunguliwa kabla ya saa 11 jioni na kufungwa baada ya saa tano usiku.

Muswada huo wa mabadiliko ya sheria ya udhibiti wa vileo [The Alcoholic Drinks Control (Amendment) Bill] uliowasilishwa na Mbunge wa Mt Elgon Fred Kapondi, ulisomwa kwa mara ya kwanza bungeni Alhamisi, Julai 21 mwaka huu. FILE PHOTO/NATION

Wandugu je hii ni hasara au ndo kampeni...??!!!

Rais Mwai Kibaki akiwasha moto meno ya tembo Jumatano Julai 20 mwaka huu katika Hifadhi ya Taifa ya Tsavo nchini Kenya, ikiwa ni jitihada za kupiga vita uwindaji haramu barani Afrika. Photo/LABAN WALLOGA/NATION
Moto ukikolea ukiteketeza meno ya tembo yaliyokamatwa sehemu mbalimbali. AFP PHOTO/Tony KARUMBA 

Tuesday, July 19, 2011

sudan kusini yazindua noti yake

Taifa jipya la Sudan Kusini limezindua fedha yake mpya ikiwa ni alama mojawapo ya utaifa.... noti hiyo inasura ya mpigania uhuru wa taifa hilo marehemu John Garang... kufuatia kuzinduliwa kwa noti hiyo.... Sudan Kaskazini nayo iko mbioni kuzindua fedha yake na kuachana na (Sudan pound) iliyokuwa ikitumiwa kabla ya kujitenga kwa Sudan Kusini. PICHA YA AFP

Wednesday, July 13, 2011

Rostam ajiuzulu nyadhifa CCM

 Aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Vijijini na waziri wa nishati na madini Nazir Karamagi akijadiliana jambo na aliyekuwa Mbunge wa Igunga Rostam Aziz wakati wa mapumziko kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 11, 2008.
Aliyekuwa Mbunge wa Igunga Rostam Aziz akiwa amejiinamia ndani ya ukumbi wa bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akilihutubia bunge mjini Dodoma Agosti 21, 2008. Wakati wa hotuba hiyo, Rostam alikaa kwa staili hiyo tangu mwanzo hadi mwisho wa hotuba hiyo. 

Mbunge wa CCM, viti maalum Kingunge Ngombale Mwiru (kulia) na jimbo la Igunga Rostam Aziz
wakiwa katika mkutano wa mashauriano baina ya wajumbe wa NEC na wabunge wa CCM uliofanyika mjini Dodoma Juni 15, 2008, chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete.

Saturday, July 9, 2011

WANAHARAKATI MPO...?!!

Katika hali ambayo kwa kweli sio ya kawaida kuonekana, mzee mmoja akimtumia mlemavu kubeba taka hapo Kimathi Lane jijini Nairobi, Kenya. Katika hili wanaharakati mna kazi..!!

Mshkaji baada ya kupakia mzigo wa taka.... anasepa taratibu.....Nadhani angelikuwa na uwezo wa kuchongesha tolori..asingelimtumia mlemavu huyo na baiskeli yake....

PICHA KUMBUKUMBU BWANA

Mzee(kulia) akiwapanga wanawe watatu (kushoto) ili awapige picha mbele ya jengo la Nation Media Group jijini Nairobi, Kenya, huku wapitanjia wakimshangaa.

FOLENI AFRIKA KAMA KAWA

Msururu wa magari ndani ya jiji la Nairobi, Kenya..... kweli Afrika hali hii kila mahali.

KUFA KUFAANA

Kweli biashara matangazo....ndani ya jiji la Nairobi, Kenya, tangazo la biashara linaloonyesha huduma zitolewazo na kampuni moja inayotoa huduma za maziko..... hapa ukipata huduma unaambiwa karibu tena....!!

sura ya Obama dili kinoma Kenya...!!

Kibao kinachoonyesha huduma ya kupiga picha za passport size kikiwa na picha kama hizo za rais Obama na mkewe Michell, jijini Nairobi, Kenya.

MAPAPARAZI KWA NEWS

Wanahabari wa Nation Media Group kutoka Mwananchi Communications, Tanzania; The Daily Monitor, Uganda na Daily Nation, Kenya wakiangalia vichwa vya habari katika magazeti mbalimbali kwa muuza magazeti jijini Nairobi.

MADEREVA BABA YAO MMOJA

Hapa askari wa kampuni binafsi ya ulinzi akikatiza bila hata ya kumstua dereva kuwa amepaki mahala pasiporuhusiwa hapo Kimathi Lane jijini Nairobi.

Hapa nilifikiri anamuendea kumbe akapitiliza




Dereva akiwa amepaki gari yake kwa Kimathi Lane jijini Nairobi, Kenya, bila hata ya kujali kuwa ameegesha mahala pasiporuhusiwa.... sijua hakuwa anajua kusoma ama aliamua kutoheshimu maelekezo yalokuwepo kwa geti.




Mambo haya ya kuchakachua si mchezo







WANAHABARI MAFUNZONI NAIROBI

Wanahabari wa Nation Media Group kutoka Mwananchi Communications, Tanzania; The Monitor; Uganda na Daily Nation wakiwa katika studio za kituo cha televisheni cha NTV, Nairobi Kenya.


Hapa wakipata maelezo juu ya shughuli za studio kutoka kwa NTV production manager, Phillip Ondeng'.


Friday, August 20, 2010

COMPUTER HARD DRIVE DISK ya 19 KWEUSI....

Hii picha ilipigwa mwaka 1956…. It's a hard disk drive back in 1956... with 5 MB of storage. Mnamo mwezi Septemba 1956, Kampuni ya IBM ilizindua a 305 RAMAC, the first 'SUPER' computer with a hard disk drive (HDD) iliyokuwa na uzito wa zaidi ya tani moja na uwezo wa kuhifhadhi data wa 5MB. At least now you have to appreciate a little more ...for the 8 GB memory stick ndani ya mufuko yako....

Tuesday, August 3, 2010

WAKINA HING HONG BALAA

JAMANI HIVI SASA HIZI BODA BODA ZISHAKUWA TATIZO BONGO VIJANA WETU WANAVUNJIKA MNO... KAMA VILE HAITOSHI.. HAWA JAMAA WAMETULETEA HIZI NYINGINE......(MALIZIA NINI KITAKACHOTOKEA)... KITENDO KAMA JINA LAKE VILE..!!

Friday, June 11, 2010

Hii shule iko wapi wajameni..?

Majina mengine ya shule... jamani ni noma... yaweza ata kuathiri wanafunzi wanaosoma hapo.....naambiwa hii skuli ipo Kisumu huko Kenya.... kwa mnaojua at ni kweli....???

Thursday, June 10, 2010

Vuvuzela kuanga kunguruma Sauz

Hii ndo raha ya soka sauz.... bila vuvuzela... soka halipigiki.... Zitaanza kunguruma kwa mwezi mmoja kuanzia hiyo kesho... wakati wa ufunguzi wa 'Weld Kap'

Hiki si kioja cha mwaka...bali ni AIBUU...

Ati hapa maafisa hawa ndo wanajionyesha kufanya kazi yao mbele ya kamanda mkubwa aliyekuwapo akishughudia mechi hiyo....
Shabiki alipandwa na mdadi na kuamua kuingia uwanjani kumkumbatia Kaka wa brazili, ambaye kwa shabiki huo anadai kuwa anamkubali kinoma....... cha kujiuliza ni kwamba jamaa huyo karuka toka eneo la jukwaa hadi kuingia kwa kiwanja(pitch) wanausalama walikuwa wapi... je angelikuwa na kisu.... ama silaha yeyote huku akiwa na nia ovu.. Tanzania ingewekwa wapi katika ramani ya soka hususan masuala ya usalama viwanjani..... Hii ni aibu....

Hapa wanausalama wanaonekana wakiwa wame-relax wakijiburudisha kwa kuangalia samba la wana brazil dhidi ya JK boys.... hawakuwa na habarin kabisaaa juu ya kuangalia usalama wa wachezaji na mashabiki wengine.... inawezekana kitendo cha shabiki hapo juu kuingia uwanjani kilitokana na hawa maafande kutokuwa sirias.....
Picha zote kwa hisani ya Jackson Odoyo....

Huu ni Unyama....

Mtoto (jina tumelihifadhi) mkazi wa Buteko nje kidogo ya mjini Kigoma, akionyesha majeraha ya moto katika nyayo zake alizochomwa hivi karibuni na mama yake mzazi, kwa madai ya kuchelewa kurudi nyumbani. Picha kwa hisani ya mdau Leonard Mubali

Hata hivyo.. kitu kimoja cha kushangaza ni kwamba matukio mengi ya ukatili wa namna kama hii dhidi ya watoto yaliyoripotiwa katika vyombo vya habari yanawahusisha au yamefanywa na akinamama. Wanawake hawa japokuwa wapo mstari wa mbele kudai na kutetea haki za watoto... kwa upande mwingine wamekuwa wakididimiza haki hizo kwa kuwatendea ukatili kama huu... hebu angalia hizi takwimu hapo chini.....

Incidents on Child abuse that shocked nation this year.
Below are some of the incidents of Child brutality by parents or guardians reported in the media recently. However, many other cases go unreported. But one may notice in such events that women, who are mothers, had been mostly reported to have carried out such cruelty to their children.
· May 17 - Police in Ruvuma arrested Asha Salum after she was allegedly slashed and seriously injured her four children using a machete. The reason was that they eat cooked rice she had anticipated to eat herself after imbibing alcohol. One child later died in hospital.
· April 30 – A woman said to be mentally retarded killed her three children with an axe in Longuo Ward in Moshi municipality.
· April 13 - Zuwena Mahamudu, 29, used a red-hot knife to burn her eight-year old Standard two son’s feet for alleged mischief.
· April 19 – A child left as a guarantee for a borrowed dress by her mother in Arusha was seriously burnt in her private parts to compensate for the delay by her mother to return the said piece of cloth.
· April 16 – A 68-year old Amina Mughubi was jailed for three years for burning her three-year old daughter in her private parts using a boiled egg over superstition.
· March 4 - Jesca Maiko, 20, a resident of Geita District in Mwanza Region was arraigned after she strangled to death a three-year old co-wife’s daughter.
· March 11 – A 37-year old Bar maid at Buguruni in Dar es Salaam severely cut her daughter’s legs, hands and buttocks after she forgot to close a door when she went to sleep.
· February 8 - A step mother at Lwega village in Rukwa region severely beat a 7-years old step daughter after she had cooked vegetable seeds. She then hung her up-side-down on a tree where she later died.
· January 13 - A five-year old girl died in Mwanza municipality of injuries sustained after was severe beaten by her mother for soiling her clothes.
· January 8 - Mwanisha Yahaya of Dar es Salaam’s Kimara suburb was charged for applying super glued on the private parts of her seven-year old daughter. The woman was furious on her daughter’s frequent soiling.

Source: The Citizen newpaper.



Wednesday, May 26, 2010

Sheria Mkononi......

(PICHANI CHINI) Askari wa kikosi maalum cha polisi cha (Anti-Robbery) kwa kiswanglish…(Shangazi Jambazi) mkoani Morogoro akimsikitikia kijana (aliyelala chini) baada ya wananchi wenye hasira kumpa kichapo kikali kwa tuhuma za kuiba baiskeli katika mtaa wa Azimio kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro…....(PICHANI JUU) ..Hata hivyo kijana hiyo hatoweza kushughudia fainali za kombe la dunia mwezi ujao… kwani ndo keshaaga dunia…Hapo akipakizwa katika Londo la Polisi kuelekea mochwale….
Picha hizo kwa hisani ya mdau Juma Mtanda… unaweza kumcheki katika http:/jumamtanda.blogspot.com