Saturday, February 7, 2009

Wazee wa Ngwasuma

wazee wa ngasuma wakishambambulia jukwaa ndani ya kilimani mjini Dom
Shabiki mzuka umepanda apeleka mkono .........

Nyoshi akinadi CD yake......

Sakata la kinasa sauti chumba ni Dr. Slaa

Afisa wa polisi akikagua kifaa kilichokutwa chumbani kwa Dr. Slaa katika Hoteli ya Fifty Six mjini Dodoma.Pichabni chini ni kifaa hicho aina ya Edic Mini Tiny

Wataalam wa teknohama kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini wamethibitisha kuwa kifaa kilichokutwa kwenye chumba cha kulala cha Mbunge wa Karatu, Dk. Willbrod Slaa (Chadema) ni kinasa sauti.

Kifaa kama hicho pia kilikutwa chumbani kwa Mbunge wa Konde, Ali Tarab Ali kwenye hoteli ya Fiftysix ambayo wabunge wote wawili wamepanga wakati huu ambao wanahudhuria mkutano wa 14, wa bunge unaoendelea mjini hapa.

Vifaa hivyo viligundulika Alhamisi iliyopita vikiwa vimetegeshwa kwenye chaga za vitanda wanavyolalia.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Omar Mganga aliwaambia waandishi wa habari kwamba vifaa hivyo vya kielektroniki vina uwezo wa kurekodi kwa muda wa saa 10 lakini hawawezi kuchukua picha.