Tuesday, January 13, 2009

Jamani mjihadhari na Madereva wa Taxi Dom

Hii mtuka.... ina tinted ndo ilikuwa ikifanza mambo ..... hiyo picha ya chini ni jinsi walivyokuwa wakiziba na nguo kuficha namba baada ya kufanya uhalifu...... soma kipande hicho hapo chini kinachofuata upate niuz ilivyokuwa....
Kwa siku kamba mbili mfululizo majamaa hao waliokuwa takrina watatu wamewaliza akinadada na kinamama kibao.... idadi ya waliokwenda kuripoti polisi juu ya uhalifu hui ilifikia saba....

Jamaa hao waligundua kuwa wanawake ni 'weak and easy target'... basi hujifanya ama wanawapa lift au wanatoa huduma ya tax....

Wakishapanda kinadada hao... na kueleza wanapoelekea... majamaa hao huunganisha juu kwa ju hadi eneo ambalo halina raia kwa wingi na kuwakaba na kuwapora kinadada hao simu, fedha na vidani.

Kwa mujibu wa wanaotuangalizia usalama wa makao makuu yetu.... mtu mmoja ameshatiwa mbaroni kuhusiana na matukio hayo......

Jamaa huyo alikwenda polisi kutoa ripoti kuwa gari yake imeibwa na ndipo polisi walipopata mashaka nae na kumbana zaidi... hatimaye akakiri kuwa alihusika...... gari hiyo ilipopatikana ilikuwa na kitambaa ambacho kilikuwa kikitumika kufunika namba za usajili za nyuma.... damu kidogo katika kiti cha nyuma zilizotoka puani kwa dada mmoja wakati wa zoezi la kumkaba.... pia ilipatikana grander moja walioporwa kimamama wengine na hao hao jamaa.....

Vitu hivyo vyote pamoja na huyo dereva aliweza kutambuliwa na wahanga wa matukio hao wakati wa gwaride la utambulisho..... Msako unaendelea kuwatavuta wenziwake waliokuwa wakitekeleza pamoja uhalifu huo......

Jamani epukeni lift za magari zizisokuwa za kichwa wala miguu... hususan kwa akina dada.... na kwa ushauri wa bure... unapokodi taxi kuwa makini kungalia waliyomo ndani...... usikubali dereva akakwambia kuwa yupo na konda wake katika taxi ..... tani kakambia taxi inaendeshwa au inawahudumu wawili...... iamin zaidi ya dereva pekee.........

ALIYEJUFANYA MTOTO WA JK KORTINI...

Kijana wa miaka 27, Rashid Twali (mbele) mkazi wa Dsm akisindikizwa kwa kortini kujibu mashitaka ya kujifanya mtoto wa JK ili kujipatia nafasi ya mafunzo katika kambi ya JKT Makutupora mkoani Dodoma
Rashid Twalib akiwa ndani ya mahakama
Hapa akirejeshwa rumande baada ya kesi ambayo imeahirishwa....... ila nduguzangu... jinsi ya kupata hizi ajira milioni moja zilizoahidiwa kaaaz kwelkwel.......!!!


Kwa Ufupi... kijana huyo alisonga hadi kambini Makutupora ambapo alipofika kwa geti alimtonya ofisa incharge kwa geti kuwa yeye ni mwana wa JK na kwamba amekuja ili kujiunga na mafunzo ya awali ya JKT kwa kambi hiyo kwani hata CDF anahabari zake.

Sajent aliyekuwepo kwa zamu hapo kwa geti alipata mashaka kidogo akawasiliana na makamanda wake ambao nao waliwasiliana na hedikotaz kupata uhakika, na huko wakawasiliana na wale jamaa wenye jengo lenye kuta nyeupe pembezoni mwa bahari ya hindi kama unaenda vile kwa kushoto.

Jamaa walipowasiliana na mzee mwenzangu ikawa sivyo hivyo, ikabainika kuwa mshkaji anafunga kamba.... hapo ndo soo likaanza na jamaa kufunguliwa chajez.......

Wee huoni hiyo alama

Askari wa Usalama barabarani akimuonya dereva baada ya kukiuka alama ya usalama barabarani (kushoto) inayomuonyesha kuwa hiyo ni njia moja tu..... Hawa ndio madereva wetu wa bongo.....

Hii ndo bongo bwana.....!!

Mshkaji akila ride mitaa ya Dom huku kapakia abiria wawili kinyume na sheria za usalama kwa road hususan kwa vyombo kama hicho kwa picha........