Saturday, January 17, 2009

Ajali mingine bwana...!!!

Sura ya lori ikiwa imekunja ndita baada ya kugonga nguzo ya umeme eneo la bahi road.....
Kitara kimeingia nyuma ya lori hilo...... hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo......

Uzembe wakati mwingine soo...

Kontena likiwa limeanguka katika kipleft kwenye barabara ya darisalam rodi.... ingawa halikuleta madhara... inaonyesha kuwa halikuwa limefungwa ipasavyo katika lori lilimokuwa.... hata hivyo baaada ya kuangakua hapo... lilikaa kwa takriban siku tatu... jambo ambalo lingeweza kusababisha ajali nyingine... lakini nadhani wahusika waliona kuwa ni sawa tuu....

Watoto wa mitaani ni tatizo kichizi dom

Kijana aishie katika mazingira magumu akiwa amelala katika bustani ya Nyerere mjini Dodoma. Idadi ya watoto kama hawa inazidi kuongezeka mkoani Dodoma ambapo takwimu zinaonyesha kuwa kuna zaidi ya watoto elfu 14 wanaoishi katika mazingira magumu mkoani humu, ambapo asilimia 62 ya idadi hiyo bado wapo mitaani.