Friday, January 23, 2009
Matatizo ya maji vijijini.......
Ndo kama hivyo tena mifugo nayo humo humo.....
Sijawa na uhakika iwapo hali hii ni salama kwa afya ya wanadamu......
Mambo ya Gadhafi
Chadema kuwasilisha hoja binafsi bungeni
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeeleza nia yake ya kuwasilisha bungeni hoja binafsi inayolenga kuilazimisha serikali kuhakikisha hakuna mtoto atakayekosa fursa ya kusoma kwa sababu ya umasikini wa wazazi wake.
Hatua hiyo ya Chadema imekuja huku wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Katika taarifa yake iliyoitoa jana jijini Dar es Salaam, Chadema imeeleza kusikitishwa kwake na utaratibu wa kudahili upya wanafunzi wa shahada ya kwanza unaoendelea UDSM kutokana na kile ilichokieleza kuwa utaratibu huo ni batili kwa kuwa unakiuka mchakato mzima wa udahili ambao hufanywa na vitivo vinavyotakiwa kuhakiki fomu za mwombaji na kuangalia vigezo, vikiwemo ufaulu wa mwanafunzi katika matokeo ya kidato cha sita au sifa zinazofanana na hizo.
Imeongeza kuwa mwanafunzi akishapata udahili, husajiliwa na si kwamba kinachofuata ni udahili mwingine
Karibu theluthi mbili ya wanafunzi waliorejeshwa nyumbani baada ya chuo hicho kufungwa kutokana na mgomo wa kupinga sera ya uchangiaji gharama za elimu, hawataweza kuendelea na masomo baada ya kutokamilisha masharti ya kurejea chuoni, ikiwa ni pamoja na kulipa sehemu ya ada
Bunge kuanza Dom
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Taarifa ya Kamati ya Uongozi ya Bunge imeitaja miswada hiyo kuwa Muswada wa Sheria ya Pembejeo (Fertilizers Act, 2008); Muswada wa Sheria ya Kanuni za Vinasaba vya Binadamu (The Human DNA Regulation Act, 2008) na Supplementary Appropriation Act, 2009 na hatua zake zote.
Miswada itakayosomwa kwa mara ya pili kuwa ni Muswada wa Sheria ya Afya ya Jamii, Muswada wa Sheria ya Wanyamapori ya Mwaka 2008, Muswaada wa Sheria ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, Sheria ya Viwango wa Mwaka 2008 na muswada wa kufanya marekebisho kwenye sheria mbalimbali wa mwaka 2008.
Maazimio matatu ya Bunge yanayotarajiwa kupitishwa ni pamoja na Azimio la Kuridhia Itifaki ya Kuanzisha Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika Mashariki; Azimio la Itifaki ya Jumuia ya afrika Masahariki kuhusu kuanzishwa kwa Chombo cha Kusimamia Usalama na Ulinzi wa Anga-2007 na Azimio la Kuridhia Itifaki kuhusu Maendeleo ya Jinsia ya Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC).