Sunday, July 24, 2011

RIP Bro Danny Mwakiteleko

Kwa kweli it is so sad.... sometimes unaweza sema God is not fair... but that is how it is...tulikaa nae tarehe July 3 usiku pamoja na Bukuku na jamaa wengine wawili... hii ndo ilikuwa last time nimeiona sura ya Danny......inasikitisha lakini hatuna jinsi.... nimejaribu kuangalia katika facebook... jinsi jamaa na marafiki walivyoguswa na msiba huu...rest in peace Bro...


Mpoki Bukuku: they say danny is no longer, sitaki kuamini! inauma sana!
Geoffrey Ng'humba: Saa ngapi sasa alipofariki? maana taarifa za magazeti ya asubuhi zimesema alitembelewa na rais na kwamba hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri? Oooh God! R.I.P. Danny.
Tausi Mbowe: bukuku inauma ndugu yangu sitaki kuamini kama Chifu Danny niliyemfahamu since 2001 sasa hatunaye, ndio hivyo tumuombee tu Mungu amlaze pema peponi kwani mbele yake nyuma yetu
Reginald Miruko: Kwaheri Kamanda Danny Mwakiteleko. Umetangulia kutuandalia makazi. Tulikupenda sana, lakini Mungu amekupenda zaidi. Ulikuwa kioo kwenye taaluma ya habari, tumejifunza mengi kutokana na ujuzi wako. Kifo chako kiwe chachu ya kupambazo na ajali za barabarani zinazoongezeka kila kukicha. Poleni wanahabari, wahariri, familia ya Mwakiteleko, ndugu na marafiki. Mungu ametoa, Mungu ametaa, jina lake lihimidiwe.
Teddy Mapunda RIP Danny Mwakiteleko 'You’ll be missed by SBL Team and will bring tears to everyone. It’s terrible when a person’s life becomes shorten by the quickest moments with so much to live for. You have brought happiness and joy to many people, for that is a true blessing for one to live for. R.I.P Danny
Teddy Mapunda Yes it is indeed! We were together in Arusha Moshi less than a week ago during editors Forum! This is the reminder from Allah that life is too short and we need to love each other and celebrate life together
Cecilia Mhina Ooh! Poleni sana jamani miaka ya mwanadamu duniani si mingi, Mungu huchuma ua lake wakati wowote apendao Mungu ailaze Roho ya Danny mahali pema Amen!
Moshi Goodluck Poleni sana familia ya Danny Mwakiteleko na wafanyakazi wa New Habari (2006) Ltd ,ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito.I will really miss his news from RAI magazine.Rest in Erternal peace my friend Danny!!
Zena Chande Ndugu yangu, matonya aliimba dunia mapito, tuwaombeni waliokufa waende salama, mimi na wewe hatujui siku yetu lini, pumzika kwa amani kaka Danny 'Patna', siku moja tutakutana
Adam Fungamwango Poleni sana wote walioguswa na msiba huu ndugu jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzake na hata sisi wenyewe waandishi! Ni kweli amekwenda Danny inauma sana, itabaki historia yake!
Benjamin Thompson Ooooh God Ooooh God why call our brother Danny Mwakiteleko now the time when we need him most!!May you please rest his soul in your eternal peace
Lwaga Mwambande Kazi ya Mungu haina makosa. Tumkumbuke Danny kwa mema yote aliyoyatenda wakati alipokuwa pamoja nasi.
Sudi Mnette Kazi ya Mungu!!
Peter Mgongo Ni msiba mkubwa kwa familia na jamii ya wana habari kwa ujumla, poleni wanafamilia wa marehemu Danny mwakiteleko mungu
awafariji ni mipango yake

Mroki T Mroki Kuna picha nimeziweka bloguni kwangu unaweza lia. Nikama alikuwa akituaga kule Arusha last week.
Bernard Rwebangira Duhh! nimeisikia muda c mrefu, RIP Danny!
Leah Mwainyekule He will surely be missed. So, so, so, sad jamani. Mwee!
Neema Mbuja Jaman mimi kama mwanahabari nimesikitishwa sana jamani sisi tulikupenda mungu amempenda zaidi
Rose Athumani Hee Mroki, kweli!!!Mungu amlaze mahala pema peponi!!! Still can't believe it!!!!
Geoffrey Ng'humba Pia tumwombee mwenzetu ndg. Kulekana, Mhariri msanifu wa DAILY NEWS ambaye anaumwa na amelazwa katika hospitali ya H. H. Agakhan Dar es Salaam. Mungu amwondolee adhabu ya maumivu na amjalie uponyaji wa haraka, Amen.
Exuper Kachenje Mungu ndiye hakimu na daima kazi yake haina makosa, Danny kwangu alikuwa mwalimu, nakumbuka alivyoniongoza kujiamini katika kazi yangu na kuwa makini. Katika hilo nitamkumbuka daima. Yeye ametangulia na kila mmoja na njia yake, lililo kubwa ni kumwombea Mwenyezi Mungu ampokee katika nuru ya uso wake mtakatifu apumzike kwa amani, Amina!!
Ibrahim Bakari Dah! Kamanda ametoweka, alikuwa si mhariri tu, pia ni kiongozi kwa waandishi, alikuwa mwalimu, alikuwa mtu wa changamoto katika uandishi wa habari. Kilichobaki tufuate yake mazuri. Mungu akupe amani ya milele, Danny.
Joseph Zablon Wengi tuliopitia katika mikono yake hatukutoka tupu, kuna ujumbe aliuleta duniani, amemaliza kazi yake na sasa kaenda kupumzika. Mungu ailaze mahali Pema Peponi Amina.....
Simba Deogratias RIP Danny.