Saturday, January 31, 2009

Magufuli alia na wavuvi haramu....

Waziri wa Mifugo na Manendeleo ya Uvuvi, John Mgufuli akitoa tamko juu ya kuanza kwa operesheni ya miezi sita ya kupambana na uvuvi haramu na uvushaji wa mazao ya samaki mipakani. Operesheni hiyo inaanza Januari 30 mwaka huu. Picha na Jube Tranquilino

Mzindakaya amlipua bomu jingine....


Mbunge wa Kwela (CCM), Dk Christant Mzindaka, akiwasilisha hoja binafsi bungeni mjini Dodoma jana juu ya kuingiliwa kwa mamlaka ya bunge kulikofanywa na serikali kupitia wizara ya maliasili na utalalii.

Mzindakaye ameeleza kusikitishwa na uzembe uliofanywa na Waziri wa Maliasili, Shamsa Mwangunga kwa kuwaongezea muda wamiliki wa vitalu vya uwindaji katika hifadhi za taifa kinyume na maagizo ya bunge.

Akitoa maeleo hayo kupitia hoja yake binafsi Mzindakaya alisema kuwa Waziri alikiuka agizo la bunge la kufuta vibali vya uwindajidhidi katika maazimio ya bunge yaliyomtaka kusitisha umiliki wa vitalu vya uwindaji wa kitalii mwishoni mwa mwaka jana na badala yake akawaongezea muda wawindaji hadi mwaka 2012.

Hoja ya Dk Mzindakaya, ambayo iliungwa mkono na wabunge wengi, ilikuwa inaweka wazi kuwa bunge liliamuru vibali vilivyokuwa vinatumika viishie 2009 ili kuanzia 2010 taratibu mpya zisizo za kuiba mapato ya serikali zitumike.

Mzindakaya alilieleza bunge kuwa kwa Waziri Mwangunga alipuuza maazimio ya bunge na kusikiliza ushawishi wa matajiri hao wa kigeni wanaofanya biashara na raslimali za nchi, kupitia vitalu walivyomilikishwa na hatimaye akawaongezea miaka miwili hadi 2012.
Mwangunga aliamriwa kusimamisha vibali vilivyotolewa na wizara yake kwa wawindaji badala ya kuisha mwaka 2012 vifikie ukomo 2010, ili kuanzia hapotaratibu mpya za uwindaji zianze kutekelezwa.