Tuesday, November 15, 2011

MVUA YALETA DHAHAMA UWANJA WA NDEGE MWANZA

Ndege ya Shirika la PrecisionAir ikiwa katika maji katika uwanja wa Ndege wa Mwanza ambao ulijaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha jana (Jumatatu).
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika uwanja wa Ndege wa Mwanza hiyo jana (Jumatatu) baada ya mvua kuleta dhahama. 
Uwanja wa Ndege wa Mwanza ukiwa umejaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha. Uwanja huo ulifungwa kwa takriban saa sita. Kiasi cha Abiria wapatao 200 waliathirika na hali hiyo. Picha/ RAY NALUYAGA

LEMA APATA DHAMANA

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akitoka mahakamani baada ya kupata dhamana jana (Jumatatu). Mbunge huyo alikaa rumande kwa takriban siku 14 baada ya kukataa dhamana ikiwa ni njia ya kuonyesha kutoridhishwa kwake na vitendo vya vyombo vya dola kumuandama. PICHA/  FILBERT RWEYEMAMU

ZOEZI LA KUONDOA KWA NGUVU WAKAZI ENEO LA MAKAO, WILAYANI MEATU, SHINYANGA


Moja kati ya familia zilizoondolewa kwa nguvu katika eneo la hifadhi (Wildlife Management Area) lililopo eneo la Makao Wilayani Meatu Mkoani Shinyanga. Eneo hilo hutumika kwa shughuli za kitalii na uwindaji. 
Moja ya nyumba zinazodaiwa kuchomwa moto katika zoezi la kuondoa kwa nguvu wakazi katika eneo hilo. Takriban kaya 625 zinadaiwa kuishi katika eneo hilo. Picha / Zulfa Mfinanga