Thursday, February 19, 2009

Mambo ya Zimbabwe soo....!!!

Noti hii yaweza nunua kiasi hicho cha bidhaa......
Matumaini mapya kwa wananchi wa Zimbabwe baada ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu mpya kutawezesha kufikiwa kwa ufumbuzi wa mzozo wa kisiasa nchini humo na kuwezesha kuondokana na hali hii ya mfumuko wa bei na kuporomoka kwa thamani ya dola ya zimbabwe.

Mauaji haya hadi lini.....?

Tunaomba radhi kutokana na picha hizi kuwa sio nzuri machoni.....Hali hii ndiyo iliyomfanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutokwa na machozi bungeni alipokuwa alielezea juu ya mauaji hayo......

Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) aliyetambulika kwa jina la Yunis Bahati mkazi wa kijiji cha Butonga kata ya Sima wilayani Sengerema ameuawa na wauawaji kutoweka na viongo vya mwili wake.

Habari zilizopatikana kutoka wilayani Sengerema na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Jamal Rwambow zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea Februari 17 usiku majira ya saa 5:00 baada ya watu wasiojulikana walipovamia nyumbani kwao na mlemavu huyo wa ngozi na kumkata miguu yake yote miwili.

Januari 21 mwaka huu albino mwingine aliyetambulika kwa jina la Jonas Maduka (47) aliuawa saa tatu usiku na wauaji kutoweka na mguu wake ambapo alifariki kutokana na kutokwa damu kutoka katika jeraha lake la mguu.

Hili ni tukio la pili kutokea Kanda ya Ziwa tangu Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofanya ziara maeneo hayo na kutoa maagizo mazito juu ya jinsi ya kukabiliana na wauaji wa Albino.

Picha hizi kwa hisani ya mwanaglobu maarufu.....