Katibu Mkuu wa UWT mkoa wa Manyara, Verosa Mjema (chini) na Katibu muktasi wake Riziki Rashid Chikoko (juu)
Katibu Mkuu wa UWT Mkoa wa Manyara Verosa Mjema pamoja na katibu muktasi wake Riziki Rashid Chikoko wamejeruhiwa vibaya baada ya kupata ajali ya gari katika eneo la chenene, Haneti wilayani Kondoa jana Januari 06 wakiwa njiani kuja
Kwa mujibu wa madaktari katika hsopitali hiyo, Verosa na Riziki wamepata majeraha makubwa kichwani ikiwa ni pamoja na mipasuko wakati riziki ameumia pia jicho lake la kushoto.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Jacob Chembele amesema majeruhi hao wanatarajiwa leo Januari 07 kusafirishwa kupelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa Matibabu zaidi.
Jumla ya watu watano wamejeruhiwa katika ajali hiyo ya gali iliyokuwa na watu sita wakiwahi mkutano huo.
Miongoni mwa wailojeruhiwa ni pamoja Suzan Maliki aliyeumia jicho la kushoto kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo ya mkoa, Phillemon Saigodi.
Wengine ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Manyara Elizabeth Malle na Christina Simon aliyepata majeraha madogo ambapo walitibiwa na kuruhusiwa.
Hata hivyo kwa mujibu wa Dkt. Saigodi mtu wa sita aliyetajwa kwa jina la Mama Chonjela aliyekuwa pamoja na majeruhi hao katika gari hiyo aina ya pajero hakufikishwa hospitali na haikufahamika mara moja iwapo alipata majeraha au laa.