Katika hali ambayo kwa kweli sio ya kawaida kuonekana, mzee mmoja akimtumia mlemavu kubeba taka hapo Kimathi Lane jijini Nairobi, Kenya. Katika hili wanaharakati mna kazi..!!
Mshkaji baada ya kupakia mzigo wa taka.... anasepa taratibu.....Nadhani angelikuwa na uwezo wa kuchongesha tolori..asingelimtumia mlemavu huyo na baiskeli yake....
Mzee(kulia) akiwapanga wanawe watatu (kushoto) ili awapige picha mbele ya jengo la Nation Media Group jijini Nairobi, Kenya, huku wapitanjia wakimshangaa.
Kweli biashara matangazo....ndani ya jiji la Nairobi, Kenya, tangazo la biashara linaloonyesha huduma zitolewazo na kampuni moja inayotoa huduma za maziko..... hapa ukipata huduma unaambiwa karibu tena....!!
Wanahabari wa Nation Media Group kutoka Mwananchi Communications, Tanzania; The Daily Monitor, Uganda na Daily Nation, Kenya wakiangalia vichwa vya habari katika magazeti mbalimbali kwa muuza magazeti jijini Nairobi.
Hapa askari wa kampuni binafsi ya ulinzi akikatiza bila hata ya kumstua dereva kuwa amepaki mahala pasiporuhusiwa hapo Kimathi Lane jijini Nairobi.
Hapa nilifikiri anamuendea kumbe akapitiliza
Dereva akiwa amepaki gari yake kwa Kimathi Lane jijini Nairobi, Kenya, bila hata ya kujali kuwa ameegesha mahala pasiporuhusiwa.... sijua hakuwa anajua kusoma ama aliamua kutoheshimu maelekezo yalokuwepo kwa geti.
Wanahabari wa Nation Media Group kutoka Mwananchi Communications, Tanzania; The Monitor; Uganda na Daily Nation wakiwa katika studio za kituo cha televisheni cha NTV, Nairobi Kenya.
Hapa wakipata maelezo juu ya shughuli za studio kutoka kwa NTV production manager, Phillip Ondeng'.