Wednesday, May 26, 2010

Sheria Mkononi......

(PICHANI CHINI) Askari wa kikosi maalum cha polisi cha (Anti-Robbery) kwa kiswanglish…(Shangazi Jambazi) mkoani Morogoro akimsikitikia kijana (aliyelala chini) baada ya wananchi wenye hasira kumpa kichapo kikali kwa tuhuma za kuiba baiskeli katika mtaa wa Azimio kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro…....(PICHANI JUU) ..Hata hivyo kijana hiyo hatoweza kushughudia fainali za kombe la dunia mwezi ujao… kwani ndo keshaaga dunia…Hapo akipakizwa katika Londo la Polisi kuelekea mochwale….
Picha hizo kwa hisani ya mdau Juma Mtanda… unaweza kumcheki katika http:/jumamtanda.blogspot.com

Vikundi vya uhamasishaji vyaanza ibuka ..uchaguzi huo waja...

Duuu.. kumbe hawa jamaa wanafani nyingi.......Katibu wa fedha na Uchumi wa CCM Taifa, Amos Makala akitwanga drums ambazo ni moja kati ya vyombo vya muziki vyenye thamni ya Sh10.2 milioni alivyowakabidhi kwa kikundi cha burudani na uhamasishaji cha ‘Sultani Dot Com’ kilichopo kata ya Sultani, manispaa ya Morogoro, Picha kwa hisani ya Samuel Msuya.

Mo Ibrahim kumtangaza rais bora Afrika 2010


Taasisi ya Mo Ibrahimu inatarajia kumtangaza kiongozi bora mstaafu barani Afrika kwa mwaka 2010 ambaye alichaguliwa kidemokrasia na akaiongoza nchi yake kwa kwa mafanikio katika misingi ya utawala bora.

Kiongozi huyo atajulikana Juni 14 na atakuwa wa tatu kufanikiwa kupata tuzo hiyo inayoandamana na donge nono la papo hapo la dola 5 milioni za Kimarekani (sawa na takriban Sh7.3 bilioni za Kitanzania).

Tanzania ina marais wastaafu wawili, Benjamini Mkapa aliyeongoza serikali ya awamu ya tatu (1995-2005) na Ali Hassan Mwinyi, awamu ya pili (1985-1995).

Kwa mujibu wa taarifa Ilioyotolewa na taasisi hiyo Jumatatu wiki hii, rais huyo bora mstaafu wa Afrika atatangazwa mjini London, Uingereza na kamati ya Mo Ibrahim inayoundwa na watu saba waliowahi kuongoza taasisi za kimataifa.

Miongoni mwa wanakamati hao yumo Salim Ahmed Salim aliyewahi kuwa waziri mkuu na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ya Afrika (OAU).

Licha ya kiongozi huyo kutunukiwa fedha hizo taslimu, taarifa hiyo inaeleza kwamba maisha yake yote atakuwa akipewa dola 200,000 za Kimarekani (sawa na takriban Shmilioni 260,000 za Kitanzania).

Kiongozi huyo atakuwa ni wa tatu kutunukiwa tuzo hiyo Barani Afrika tangu taasisi hiyo ilipoundwa mwaka 2007.

Waliotunukiwa tuzo hiyo ni rais wa zamani wa Msumbiji, Joaquim Chissano aliyetunukiwa mwaka 2008 na Festus Mogae wa Bostwana (2007).

Mwaka jana kamati hiyo, iliyo chini ya katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, haikumpata mshindi wa tuzo hiyo.

Taasisi hiyo inaongozwa na mfanyabiashara tajiri wa Sudan, Mo Ibrahim, ambaye amebuni tuzo hiyo kwa lengo la kuimarisha demokrasia na utawala bora Barani Afrika.

Story na Leon Bahati
Source:http://mwananchi.co.tz
Jumatano, 26 May 2010 08:48

Makamba awangurumia makatibu uwenezi CCM

Katibu Mkuu wa CCM Yusuph Makamba, akionyesha vitabu mbalimbali vya maarifa na katiba ya chama mjini Dodoma, Jumanne wiki hii wakati wa ufunguzi wa semina kwa makatibu uwenezi wa CCM kutoka mikoa yote NCHINI. Kulia ni Katibu wa Itikadi na uenezi CCM Kepteni Mstaafu John Chilighati. Picha kwa hisani ya Israel Mgusi... Soma story hapo chini.....

Makamba atamba, aonya makatibu
Jumatano, 26 Mei 2010 08:47

Habel Chidawali, Dodoma

KATIBU mkuu wa CCM, Yusufu Makamba amewaonya makatibu wa siasa na waenezi wa chama hicho, akiwataka kutonunuliwa na wagombea ubunge na akajinasibu kuwa yeye ni mtu anayekwenda na wakati hivyo hawezi kung’olewa katika nafasi hiyo.

Makamba alitoa onyo hilo jana kwenye ukumbi wa NEC Mjini hapa wakati akifungua semina ya siku tatu kwa makatibu hao ambayo itamalizika kesho.

Makamba, ambaye anajulikana kwa ucheshi, pia aliwasimamisha kwenye mkutano huo baadhi ya viongozi wa jumuiya ya wazazi wa mikoa ya Tanga, Morogoro na Dar es salaam, akiwatuhumu kuwa ni vibaraka wa wagombea ubunge.

Katika hotuba yake, Makamba alitamba kuwa njia itakayomuokoa yeye asing’oke katika nafasi yake ni uamuzi wake wa kusoma kwa bidii.

“Mimi nimesoma na ninasoma kila wakati ndiyo maana sibabaiki kabisa... hata ukiniuliza jambo lolote naweza kukuambia kutokana na ukweli kuwa ninakwenda na wakati na nitaendelea kuwa hivyo kila mara ndio maana watu wanasema kuwa ning’atuke, lakini wanaishia kutokuwa na majibu kwa kuwa ninaenda na wakati," alitamba Makamba ambaye watu walitaka aondolewe baada ya CCM kuanguka kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime.

Aliwataka Makatibu hao kutumia muda wote wa kazi zao katika kupitia vitabu mbalimbali vikiwemo vitabu na vijarida vilivyoandikwa mambo ya CCM ili kujiimarisha katika misingi mizuri ya kupambana na maswali yanayotoka upande wa wapinzani.

Makamba, ambaye amekuwa akimnadi Rais Jakaya Kikwete kuwa ndiye mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama hicho, aliwataka viongozi hao kutokuwa vibaraka wa wagombea ubunge.

Kuhusu uchaguzi mkuu ujao, mtendaji huyo mkuu wa chama tawala alisema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni "ushindi ni lazima ndani ya CCM" na kwamba hilo lazima itekelezwe chini ya usimamizi wa makatibu hao.

“Kwa hiyo mkiondoka hapa msiende kulala; hakikisheni chama kinashinda kweli maana hata tafiti mbalimbali zilizofanywa zimeonyesha kuwa CCM inakubalika kwa asimilia kubwa,” alisema Makamba.

Alisema kuwa mbali na utafiti ambao umeonyesha kuwa Kikwete anakubarika kwa asilimia 85.5, uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana ulikuwa ni kipimo tosha cha kuonyesha kuwa CCM inakubalika baada ya kushinda kwa asilimia 91.7.

Source:http://mwananchi.co.tz

S

Hii ngoma itakuwa kama ya Liyumba au..????

Watuhumiwa wa kesi ya matumizi mabaya ya madaraka katika Serikali ya awamu ya tatu,kutoka kushoto Basil Mramba, Daniel Yona na Grey Mgonja, wakijadili jambo wakati wakiwa katika chumba cha Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam Jumanne wiki hii, wakisubiri kusikilizwa kwa kesi yao.Picha kwa hisani ya Michael Matemanga

JK ahutubia bunge Afrika Mashariki

Mwenyekiti wa jumuiya Ya Afrika Mashariki, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia bunge la jumuiya hiyo jijini Nairobi Jumanne wiki hii.Kushoto ni Spika wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mheshimiwa Abdirahin Abdi.
Rais Jakaya Kikwete (Katikati) akiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdirahin Abdi (kushoto) pamoja na Spika wa Bunge la Kenya Kenneth Marende(kulia) wakiwa katika viwanja vya Bunge la Kenya Muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili na kupigiwa wimbo wa taifa.

Rais Mwai Kibaki wa Kenya akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Nairobi jJumanne wiki hii kwa mazungumzo mafupi muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kulihutubia bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Picha zote kwa hisani ya Ikulu