Monday, August 22, 2011

Watu 23 wafa katika ajali Mbooni huko Machakos nchini Kenya

Baadhi ya wananchi wakiangalia mabaki ya basi lililopinduka na kutumbukia katika Mto Uwaani, karibu na Mbumbuni sokoni, tarafa ya Mbooni huko Machakos, Kenya, Jumamosi usiku. Watu 23 wakimemo ndugu wanne wa familia moja, waliokuwa wakitoka katika shughuli ya kutoa posa na mahari, wamepoteza maisha katika ajali hiyo ambayo inaelelezwa kuwa ni moja kati ya ajali mbaya zaidi za barabarani kutokea nchini Kenya mwaka huu.  Watu wengine 36 wamejeruhiwa katika ajali hiyo. Source: Daily Nation/ Photo Phoebe Okall

Polisi mkoani Kigoma yakamata 52 katika operesheni

 Bangi iliyokamatwa na polisi mkoani Kigoma
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linawashikilia watu 52 kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za ujambazi wa kutumia silaha na wizi wa vocha za simu za mkononi zenye thamani ya karibu shilingi milioni 63.2.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP Fraisser Kashai, amesema kuwa watuhumiwa 21 wamekamatwa katika wilaya ya Kigoma mjini, watuhumiwa 18 wamekamatwa katika wilaya ya Kasulu na wengine 13 katika wilaya ya Kibondo. Picha/ Pardon Mbwate, PT