Saturday, January 24, 2009

Usafiri reli ya kati

Baadhi ya wasafiri wakiwahi kupanda katika sehemu ya injini(kichwa) cha treni katika stesheni ya Dodoma wakielekea mikoa ya Tabora, Kigoma na Mwanza....
Wengine hawakuwa na pakuweka mizigo yao zaidi ya kuipachika katika maungio ya mabehewa.....
Ndani kumejaa kinoma... inabidi wengine waning'inie katika milango.....
Kujaza abiria kupita kiasi ndio mtindo wa kila siku.... lakini kwa wasafiri nao.... wanaona bora kufika salama tu....
Kero hii imekuwa ni kubwa na ya muda mrefu.... ijapokuwa imepigiwa kelele na wadau mbalimbali wakiwemo wabunge........ Mambo haya yataisha lini....?

Chuo Kikuu cha Dodoma....si mchezo....

Sura ya mbele ya jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho ujenzi wake ukikamilika kitakuwa ni mojawapo ya vyuo vikuu vikubwa katika Ukanda wa Afrika....
Jengo hili zamani lilijulikana kama Ukumbi wa Mikutano wa Chimwaga...
Mojawapo kati ya maeneo ambapo vitivo vinaendelea kujengwa... hadi sasa kuna vitivo sita ambavyo kila kimoja kitajitegemea kwa kila kitu.....
Baadhi ya mabweni.... hili pichani ni la kitivo cha sayansi ya jamii.......