Thursday, February 19, 2009

Mauaji haya hadi lini.....?

Tunaomba radhi kutokana na picha hizi kuwa sio nzuri machoni.....Hali hii ndiyo iliyomfanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutokwa na machozi bungeni alipokuwa alielezea juu ya mauaji hayo......

Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) aliyetambulika kwa jina la Yunis Bahati mkazi wa kijiji cha Butonga kata ya Sima wilayani Sengerema ameuawa na wauawaji kutoweka na viongo vya mwili wake.

Habari zilizopatikana kutoka wilayani Sengerema na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Jamal Rwambow zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea Februari 17 usiku majira ya saa 5:00 baada ya watu wasiojulikana walipovamia nyumbani kwao na mlemavu huyo wa ngozi na kumkata miguu yake yote miwili.

Januari 21 mwaka huu albino mwingine aliyetambulika kwa jina la Jonas Maduka (47) aliuawa saa tatu usiku na wauaji kutoweka na mguu wake ambapo alifariki kutokana na kutokwa damu kutoka katika jeraha lake la mguu.

Hili ni tukio la pili kutokea Kanda ya Ziwa tangu Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofanya ziara maeneo hayo na kutoa maagizo mazito juu ya jinsi ya kukabiliana na wauaji wa Albino.

Picha hizi kwa hisani ya mwanaglobu maarufu.....

No comments: