Thursday, December 31, 2009

Ni kutokujua kusoma au ukaidi...?


Mfanyabiashara ndogondogo akiuza ndizi katika eneo linalokatazwa kandokando ya barabara ya kuelekea hospitali kuu ya Mkoa wa Dodoma. Lakini kwa nyuma askari nao wakipita na hamsini zao, ingawa bango linalokataza biashara limeandikwa kuwa na amri halali..... Hapo sasa....

1 comment:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Tunajua kwa nini ni marufuku kufanya biashara katika eneo hilo? Aliyeweka hii amri ana njia za kuhakikisha kwamba amri yake inatekelezwa; au amebandika bango tu na kutokomea zake? Pengine hata hakumbuki kama aliweka amri kama hiyo katika eneo hilo. Inawezekana pia kwamba hilo eneo ndilo lenye wateja wengi - watu wanaokwenda hospitalini kwa sababu mbalimbali. Na mama huyu anategemea biashara hii ili kujikimu.

Tusisahau pia kwamba tuna utamaduni wa kutozingatia sheria hasa hizi ndogo ndogo (hata kubwa kubwa kama una ubavu). Umeshaona kibao kimeandikwa "usitupe takataka hapa" na wakati huo huo taka ndiyo zimejaa pale? Au "usikojoe hapa" na ukiangalia nyasi zinazozunguka kibao hicho zimeungua kwa mkojo? Pointi siyo kuweka amri kwenye mabango, suala ni utekelezaji wake. Na kwa hili jamii yetu inapata ziro.

Tusimlaumu huyu mama, mwache auze ndizi zake halafu jioni akanunue mkate watoto wake wakale!