Wanywa vileo nchini Kenya watakuwa na kila sababu ya kufurahia iwapo bunge la nchi hiyo litapitisha muswada wa sheria unaolenga pamoja na mambo mengine kuongeza muda wa kufunguliwa kwa sehemu zinazouza vileo (baa) kutoka muda wa sasa wa saa 6 hadi kufikia saa 12 kwa siku.
Kwa sheria iliyopo sasa, baa hufunguliwa kuanzia saa 11 jioni na kufungwa saa tano usiku kwa siku za kazi (week days). Iwapo muswada huo utapita, inamaana kuwa baa zitafunguliwa kabla ya saa 11 jioni na kufungwa baada ya saa tano usiku.
Muswada huo wa mabadiliko ya sheria ya udhibiti wa vileo [The Alcoholic Drinks Control (Amendment) Bill] uliowasilishwa na Mbunge wa Mt Elgon Fred Kapondi, ulisomwa kwa mara ya kwanza bungeni Alhamisi, Julai 21 mwaka huu. FILE PHOTO/NATION
No comments:
Post a Comment