Baadhi ya wananchi wakiangalia mabaki ya basi lililopinduka na kutumbukia katika Mto Uwaani, karibu na Mbumbuni sokoni, tarafa ya Mbooni huko Machakos, Kenya, Jumamosi usiku. Watu 23 wakimemo ndugu wanne wa familia moja, waliokuwa wakitoka katika shughuli ya kutoa posa na mahari, wamepoteza maisha katika ajali hiyo ambayo inaelelezwa kuwa ni moja kati ya ajali mbaya zaidi za barabarani kutokea nchini Kenya mwaka huu. Watu wengine 36 wamejeruhiwa katika ajali hiyo. Source: Daily Nation/ Photo Phoebe Okall
No comments:
Post a Comment