Mkufunzi wa Shule ya Udereva ya Dodoma Ondi Nyarari (wa pili kushoto) akimpa maelezo Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwasa (kulia) juu ya kitabu maalum chenye maelezo juu ya alama za barabarani kwa waendesha pikipiki wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Dodoma Jumatatu wiki hii.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi (kulia) akipokea maelekezo kutoka kwa Mkufunzi wa Shule ya Udereva ya Dodoma Ondi Nyarari kuhusu kozi fupi za madereva wa pikipiki (boda boda) katika wiki ya nenda kwa usalama. Mkuu huyo wa Mkoa alizindua wiki hiyo Jumatatu wiki hii mkoani Dodoma. Picha/ Habel Chidawali
No comments:
Post a Comment