Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma Zelothe Stephen akionyesha moja ya noti bandia za Sh10,000 zilizokamatwa Jumatatu mkoani humo. Picha/Habel Chidawali
Jeshi la Polisi Mkoani hapa linawashikilia watu wawili kwa kosa la kukamatwa na noti bandia ambazo thamani yake ni Sh 250,000.
Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma Zelothe Stephen aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu wiki hii kuwa nyingi kati ya fedha hizo zilikuwa ni noti za Sh 5,000 na Sh10,000.
Baadhi ya noti zilizoonyeshwa kwa waandishi wa habari zilikuwa na namba zinazofanana ikiwemo noti za Sh10,000 ambazo zaidi ya noti 5 zilikuwa na namba moja iliyosomeka AC 0011680 huku noti 8 za Sh5,000 zikisomeka kwa namba moja ya BH 0012036.
Zelothe aisema upelelezi kamili wa kesi hiyo unaendelea ili kubaini watengenezaji pamoja na mashine zinazotumika kwa ajili ya kutengeneza noti hizo.
No comments:
Post a Comment