Friday, January 23, 2009

Bunge kuanza Dom

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaanza Mkutano wake wa 14 mjini Dodoma Jumanne wiki ijayo (Januari 27) mwaka huu ambapo miswada mitatu mipya itasomwa na maazimio matatu yanatarajiwa kupitishwa.


Taarifa ya Kamati ya Uongozi ya Bunge imeitaja miswada hiyo kuwa Muswada wa Sheria ya Pembejeo (Fertilizers Act, 2008); Muswada wa Sheria ya Kanuni za Vinasaba vya Binadamu (The Human DNA Regulation Act, 2008) na Supplementary Appropriation Act, 2009 na hatua zake zote.


Miswada itakayosomwa kwa mara ya pili kuwa ni Muswada wa Sheria ya Afya ya Jamii, Muswada wa Sheria ya Wanyamapori ya Mwaka 2008, Muswaada wa Sheria ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, Sheria ya Viwango wa Mwaka 2008 na muswada wa kufanya marekebisho kwenye sheria mbalimbali wa mwaka 2008.


Maazimio matatu ya Bunge yanayotarajiwa kupitishwa ni pamoja na Azimio la Kuridhia Itifaki ya Kuanzisha Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika Mashariki; Azimio la Itifaki ya Jumuia ya afrika Masahariki kuhusu kuanzishwa kwa Chombo cha Kusimamia Usalama na Ulinzi wa Anga-2007 na Azimio la Kuridhia Itifaki kuhusu Maendeleo ya Jinsia ya Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC).


No comments: