Tuesday, January 13, 2009

Jamani mjihadhari na Madereva wa Taxi Dom

Hii mtuka.... ina tinted ndo ilikuwa ikifanza mambo ..... hiyo picha ya chini ni jinsi walivyokuwa wakiziba na nguo kuficha namba baada ya kufanya uhalifu...... soma kipande hicho hapo chini kinachofuata upate niuz ilivyokuwa....
Kwa siku kamba mbili mfululizo majamaa hao waliokuwa takrina watatu wamewaliza akinadada na kinamama kibao.... idadi ya waliokwenda kuripoti polisi juu ya uhalifu hui ilifikia saba....

Jamaa hao waligundua kuwa wanawake ni 'weak and easy target'... basi hujifanya ama wanawapa lift au wanatoa huduma ya tax....

Wakishapanda kinadada hao... na kueleza wanapoelekea... majamaa hao huunganisha juu kwa ju hadi eneo ambalo halina raia kwa wingi na kuwakaba na kuwapora kinadada hao simu, fedha na vidani.

Kwa mujibu wa wanaotuangalizia usalama wa makao makuu yetu.... mtu mmoja ameshatiwa mbaroni kuhusiana na matukio hayo......

Jamaa huyo alikwenda polisi kutoa ripoti kuwa gari yake imeibwa na ndipo polisi walipopata mashaka nae na kumbana zaidi... hatimaye akakiri kuwa alihusika...... gari hiyo ilipopatikana ilikuwa na kitambaa ambacho kilikuwa kikitumika kufunika namba za usajili za nyuma.... damu kidogo katika kiti cha nyuma zilizotoka puani kwa dada mmoja wakati wa zoezi la kumkaba.... pia ilipatikana grander moja walioporwa kimamama wengine na hao hao jamaa.....

Vitu hivyo vyote pamoja na huyo dereva aliweza kutambuliwa na wahanga wa matukio hao wakati wa gwaride la utambulisho..... Msako unaendelea kuwatavuta wenziwake waliokuwa wakitekeleza pamoja uhalifu huo......

Jamani epukeni lift za magari zizisokuwa za kichwa wala miguu... hususan kwa akina dada.... na kwa ushauri wa bure... unapokodi taxi kuwa makini kungalia waliyomo ndani...... usikubali dereva akakwambia kuwa yupo na konda wake katika taxi ..... tani kakambia taxi inaendeshwa au inawahudumu wawili...... iamin zaidi ya dereva pekee.........

No comments: